Na Mwandishi Wetu, Bumbuli
SERIKALI imetakiwa kufikia uamuzi wa haraka juu ya kumtafuta
mwekezaji mwingine wa kiwanda cha Chai, cha Mponde, kilichopo Halmashauri
ya Bumbuli, Wilayani Lushoto, ili kuinusuru chai ya wakulima
inayoendelea kuharibikia shambani kwa miezi minane sasa, tangu kifungwe.
Kiwanda hicho cha Mponde ambacho ni Umoja wa Wakulima wa Chai (UTEGA), wanamiliki asilimia hamsini, huku mwekezaji asilimia iliyobaki, kilifungwa baada ya wakulima kugoma kupeleka majani mabichi kwa madai kuwa mwekezaji huyo anawalangua.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wilayani Bumbuli, wakulima hao walisema tangu kiwanda hicho kimefungwa jana chai yao inaharibikia
mashambani na kuwapa ugumu wa maisha.
Hamis Jabiri mkulima wa Chai katika halimashauri hiyo, aliiomba serikali kuwafungulia kiwanda chao ili kunusuru maisha yao, maana wamekuwa wakiishi maisha magumu na kuongeza makali ya maisha na kuyumbisha uchumi wao.

Naye Robart Tembe, alisema baada ya kufikia uamuzi
wa kukifunga kiwanda hicho, serikali iliunda tume ili kupendekeza kuundwa kwa
uongozi wa muda katika kiwanda hicho.
"Waandishi wa habari maamuzi ya kufungwa kwa kiwanda tuliyafanya sisi wakulima kwasababu hatumtaki mwekezaji, hivyo serikali ilete mwingine na kuanza kuendesha uzalishaji na sisi tuuze chai yetu kama ilivyokuwa mwanzo,” alisema Tembe.
Akizungumzia hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Bumbuli, Beatreace Msomisi, alisema tangu kiwanda hicho kilivyoacha
kufanya kazi halmashauri hiyo imeathirika kiuchumi, kwasababu ya kiwanda hicho
kuwa tegemezi la wakulima."Waandishi wa habari maamuzi ya kufungwa kwa kiwanda tuliyafanya sisi wakulima kwasababu hatumtaki mwekezaji, hivyo serikali ilete mwingine na kuanza kuendesha uzalishaji na sisi tuuze chai yetu kama ilivyokuwa mwanzo,” alisema Tembe.
No comments:
Post a Comment