Hii ndio kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, akielezea mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika ziara yake wilayani Handeni, Korogwe na maeneo mengine ya Mkoa wa Tanga. Pia DC Muhingo alielezea tatizo la maji na kusema kuwa litapatiwa ufumbuzi kwa kutengwa kiasi cha Sh Bilioni 4 kwa ajili ya maji wilayani Handeni.....
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu pichani.
"Nashukuru
Kambi, huwa nasoma sana mtandao huu sana. Tupo kwenye maandalizi,
tumeaandaa mabasi manane ya kubeba watu; matatu toka Komsala kwenda
Handeni na matatu toka Mkata kwenda Handeni. Tumepika chakula cha
kutosha watu 2,000 ili kila anayefika asishinde
njaa. Tutakuwa na vikundi kadhaa vya burudani bila kusahau ngoma ya
selo pamoja a wapambanaji wa JKT. Tutakuwa na bendi tatu. Taarabu moja ya JKT itapiga leo usiku.Tumechelewa hamasa kwa sababu tumepata uthibitisho wa ziara siku ya Alhamisi lakini tunajitahidi watu wengi wafike. Hoja kama wengi mnavyosema ni maji na tungefurahi wananchi wakimuomba rais wao kuhusu maji. Hata hivyo, mwaka huu serikali imetenga shilingi bilioni nne kwa ajil ya wilaya ya Handeni tu.
Ni hela nyingi kutolewa kuliko wilaya yoyote nchini. hizi zinatosha kuchimba mabwawa 17, kati ya hayo mabwawa mawili yanaendelea kuchimbwa likiwamo la Mkata na Manga. Maji kutoka Wami yapo kijiji cha Kwasunga, yanakuja Manga. Serikali imekubali kutupatia fedha kwa lengo la kufufua mradi wa HTM. Mradi huo unahitaji jumla ya shilingi bilioni 136.
Hata hivyo, serikali itatusaidia fedha hizo kwa awamu. Tumeagiza mashine kwa ajili ya Sindeni na fedha tumekwishalipa shilingi milioni 50 na inatarajiwa kufika mwishoni mwa mwisho wa mwezi ujuao. Hii itauhakikishia mji wa Handeni maji ya uhakika. Natamani mmoja wenu journalism aje ili tuandike program na matatizo ya maji Handeni"
No comments:
Post a Comment