Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKURUNGENZI
Mtendaji wa Shule na kituo cha kukuza michezo ya vijana cha Alliance
School Sports Academy, James Bwire amesema timu ya Alliance inayotoka
kituo hicho ikipanda daraja, ubigwa wa Ligi Kuu utahamia jijini Mwanza.
Akizungumza
jijini Mwanza, baada ya kumalizika kwa mechi kati ya
Alliance na timu ya Chuo cha Biashara (CBE), alisema vijana wanaondaliwa
na kituo
hicho watabadilisha soka nchini na kuleta changamoto ligu kuu.
Bwire
alisema vijana wa timu ya Alliance waliopo daraja la nne hivi sasa
wanaandaliwa na kupewa mafunzo ya kimichezo ngazi ya kimataifa ndio
maana wanashinda mechi zao zote ndani na nje ya nchi.
“Kituo chetu
kinaandaa vijana wa michezo kwa malengo, unajua zipo timu zinapanda
daraja na kushiriki ligi kuu kwa kubahatisha na kushuka kwa muda mfupi,
sisi hilo hatutaki ndio maana yapo masomo ya jinsi ya kucheza mpira
uwanjani.
"Nadhani ni mara ya kwanza nchini kuona mtoto anayecheza
ligi daraja la nne anachukuliwa hadi timu ya Taifa, lakini Alliance
imefanikiwa kutoa Atanas Mdamu.
“Sasa nasema Alliance ikifanikiwa
kufikia ligi kuu, itafuta uteja wa kombe kubaki Dar es Salaam, timu hii
itabadilisha soka na mazoea yaliyopo sasa, hili nalisema kwa dhihiri
kabisa kwani historia imeanza kujionyesha,kila timu za ndani na nje
tunashinda na vikombe
tunachukua.
“Tunajua kuna watu hawataki kuona timu ndogo inakuja
kasi kama ilivyo Mbeya City ambayo kidogo imeleta changamoto , nawaomba
viongozi wake wasiwe watu wa kurubuniwa.
No comments:
Post a Comment