https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, March 28, 2014

MMJKT Mabingwa wa ngumi Mkoa wa Dar es Salaam

Bondia Hamisi Mputeni kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Victor Njaiti wakati wa mpambano wao katika mashindano ya klabu bingwa mkoa wa Dar es salaam juzi. Njaiti alishinda kwa pointi.
 Na Mwandishi Wetu
TIMU ya MMJKT jana imeibuka mabigwa wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam baada ya kuvipiku vilabu nane vilivyoweza kujitokeza kushiliki mashindano hayo na kutawazwa kuwa bingwa wa mkoa baadhi ya mabondia waliocheza fainal za mashindano hayo ni Hamisi Mrisho wa 'MMJKT' alisambalatishwa kwa pointi na bondia Oscar Richard wa 'Urafiki'   na Omari Mohamed wa urafiki akichezea kichapo kutoka kwa mwenzie John Mwambinga, na bondia anaekuja kwa kasi ya ali ya juu akitokea timu ya Ashanti ya ilala kwa sasa akichezea timu ya 'MMJKT'  alifanikiwa kumpiga John Christian wa 'Mgulani' Saleh Abdallah wa mgulani alishindwa kutamba mbele ya  Undule Langson wa Magereza.

Bondia Mohamed Chibumbuli kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdul Rashid  wakati wa mchezo wao katika mashindano ya klabu bingwa mkoa wa Dar es salaam Chibumbuli alishinda kwa pointi. 
Nae Jacobo Agusteno wa 'mgulani' alishindwa kufulukuta mbele ya Bosco Bakari wa 'MMJKT' katika mpambano mwingine uliowakutaniasha Festo Ngabo wa Magereza alishindwa kutamba mbele ya Victor Njaiti wa 'mmjkt' nae bondia Mohamedi Chibumbuli wa magereza alimsambalatisha vibaya bondia Said Saleh wa 'mavituzi'  akizungumzia maandalizi ya mabondia wa mkoa wa Mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa Dar es salaam 'DABA' Akaroli Godfrey amesema kwa sasa mabondia wa timu ya mkoa wa Dar es salaam wapo kambini wakijiandaa na mashindano ya majiji yatakayoanza Kampala Uganda April 2 mwaka huu timu hiyo ambayo ipo na makocha wazoefu wakiongozwa na David Yombayomba ,Ferdnand Nyagawa mazoezi yanayofanyika kila siku mgulani JKT, wakisaidiwa na Mazimbo Ally na Kameda Antony 

timu hiyo ina maitaji mbalimbalio ikiwemo kambi pamoja na kupeleka timu Uganda ambayo itagalimu milioni 16 kwa ajili ya kwenda kwenye mashindano hayo ambapo mpaka sasa wamenda sehemu mbalimbali ikiwemo makampuni na kwa watu binafsi hata hivyo akuna mafanikio yoyote hivyo kuwaomba wadau wa mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kusaidia timu hiyo ambayo inakabiliwa na mashindano ya majiji.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...