https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Thursday, March 27, 2014

Mwili wa marehemu, John Tupa, Mkuu wa Mkoa wa Mara waagwa rasmi leo


Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tupa, ukitolewa kwenye makazi yake kwa ajili ya taratibu nyingine za mazishi yake.

Mwili wa marehemu ukiagwa
 Waombolezaji wakiwa msibani kwa Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Mara, John Tupa.

Kutoka kushoto, ni Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Poul Kasabago, mjumbe wa NEC ya CCM, Christopher Gachuma, wakiwa msibani.

MAELFU ya wananchi wa mkoa wa Mara pamoja na mikoa jirani wakiongozwa na viongozi wa Serikali, Dini na vyama vya Siasa wameuaga mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa aliyefariki juzi asubuhi akiwa wilayaniTarime kwa shughuli za kikazi.


Akitoa salamu za rambirambi za Serikali mkoani Mara, Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Bartazal Kichinda alisema walipokea kwa masikitiko makubwa msiba wa ghafla wa mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa  kwa kuwa msiba huo umekuja wakati mchango  na usaidizi wa kiongozi huyo ukiwa unahitajika zaidi mkoani Mara.
Picha zote kwa hisani ya Shomari Binda.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...