https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, March 05, 2014

Matukio katika picha kampeni za CCM jimbo la Kalenga

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Nchemba (kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Joyce Msamba tavangu (katikati) na mgombea ubunge kupitia CCM, Mgimwa wakicheza walipofika kwenye kampeni katika Kijiji cha Kibebe. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (32), akiwapungia wananchi huku akiwa amebebwa alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mangalali,  Kata ya Ulanda, Iringa Vijijini jana mchana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akiongoza msafara wa mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa aliyebebwa walipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mangalali.
Mgimwa akiungana na wanakijiji kucheza ngoma ya asili ya kabila la Wahehe alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe, Kata ya Ulanda mchana leo.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Kalenga Tosamaganga, Kisabugo Mkemwa akitoa mahubiri ya kumuombea Mgimwa (kushoto) ili ashinde uchaguzi huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Nchemba.                                              
 
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Iringa, Aloyce Mgongolwa akisikiliza kwa makini wakati Nchemba akihutubia katika mkutano huo wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe.
Ofisa Mwandamizi wa Mawasiliano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Gabriel Athuman akinywa maji ya kisima ambayo aliyasifia kuwa ni matamu wakati wa mkutano wa Kampeni za CCM Jimbo la Kalenga katika Kijiji cha Kibebe
Akina mama wakisikiliza kwa makini wakati Mgimwa akijinaji katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kibebe leo mchana.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, Mgimwa.
Aliyewahi kuwa Mgombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki kupitia Chadema,  na Ofisa wa Chadema Makao Makuu, Mwampamba akielezea jinsi alivyoamua kujiondoa kwenye chama hicho bhaada ya kufanyiwa mabaya na uongozi wa Chadema ambacho alidai hakifai wananchi kujiunga nacho.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...