Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAFANYAKAZI 176 wa Shirika la Reli la Zambia na Tanzania
(TAZARA), wamejiunganisha kwa pamoja na kufungua tawi la klabu ya Simba, wakiwa
na shauku ya kuisaidia timu yao
kufanya vyema na wao kupata raha ya ushindi.
Baadhi ya wanachama wa Tawi la TAZARA wakisikiliza maneno ya meza ya mbele.
Uzinduzi wa tawi hilo
ulikwenda sambamba na kugawa kadi 50 za uanachama kwa wafanyakazi hao, huku
mgeni rasmi akiwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo, Swed
Mkwabi.
Swed Mkwabi, mwenye fulana nyekundu, akipiga picha ya pamoja na wanachama wa tawi la Simba la TAZARA leo jijini Dar es Salaam
Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu wa Tawi hilo jipya la Simba lililokuwa na maskani yake TAZARA,
Abdallah Sambizi, alisema kuwa kuanzishwa kwa tawi hilo
ni hatua muhimu za kuisaidia klabu yao.
Mgeni Rasmi, aliyesimama meza ya mbele, Swed Mkwabi, akisikiliza baadhi ya hoja kutoka kwa wanachama wa Simba, Tawi la TAZARA, jijini Dar es Salaam leo.
Alisema kuwa wanaamini kwa pamoja watafanya mambo mema ya
kusaidiana na viongozi wao Makao Makuu kwa ajili ya kuipaisha timu yao, ambayo kwa msimu huu
imeonekana kusua sua.
Sisi mashabiki na wanachama tunachohitaji ni ushindi tu,
hivyo naamini kwa pamoja tutashirikiana na wenzetu wa Makao Makuu ili kuipaisha
klabu yetu ndani na nje ya nchi, huku tukiepuka kuwa wasumbufu au kutoa matamko
yasiyokuwa na mashiko kwa timu yetu tunayoipenda,” alisema Sambizi.
Naye Mgeni rasmi wa uzinduzi wa tawi hilo, Mkwabi, aliwataka
wanachama na viongozi wa tawi hilo kuwa na dhamira ya kweli ya kuisaidia Simba
na sio wao kusaidiwa na klabu yao kwa kushiriki au kujitolea kwa mambo ya
kimaendeleo.
TAZARA msisubiri mlipe ada tu ya Sh 1000 kwa mwezi badala
yake muingie sasa kwa kushiriki mambo mazuri, hasa ya kununua bidhaa halali za
Simba ambapo hayo ndio maendeleo makubwa,” alisema.
Viongozi wa tawi hilo ni pamoja na Mwenyekiti Hemed Msangi,
Makamu Mwenyekiti Amri Hussein, Katibu Sambizi, Katibu Msaidizi ni Gabriel
Samson, Katibu Mwenezi ni Alfred Mdemu, Mweka Hazina ni Kijakazi Herith,
wajumbe ni Nicholaus Bukuku, Khatibu Makata, Heronima Maganga.
No comments:
Post a Comment