https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, March 12, 2014

Karibu upitie maoni ya mjadala wa migogoro ya ardhi katika group la Handeni Kwetu wiki iliyopita


MHANDENI SONYO....
HABARI za leo ndugu zangu wooote. Tunashukuru kwa kuendelea kuwa na afya njema. Wale wanaosumbuliwa na maradhi tunawaombea mpate afya njema ili tuendelee na ujenzi wa Taifa letu. Leo ni siku nyingine, tunaingia katika mjadala wetu. Leo tunaangazia migogoro ya ardhi na changamoto zake. Katika maeneo mengi ya Tanzania, hususan wilayani Handeni kuna migogoro mingi ya ardhi. Ikumbukwe kuwa, migogoro ya ardhi inaweza kuzalisha vurugu na kusababisha mauaji pia. Tafadhali sana, Mhandeni Sonyo, katika migogoro ya ardhi unajua jinsi gani sakata hili linaweza kutatuliwa kiungwana. Nini kifanyike ikiwa ni pamoja na wakulima na wafugaji ambao nao ndio chanzo cha migogoro yao? Handeni tumeathirika kwa kiasi gani na vipi tunaweza kushirikiana wananchi, viongozi na wadau wengine wa ardhi kuweka mambo sawa? Karibu ufunguwe mjadala wetu na sisi tutaendelea kuchangia kwa kufuata mitiririko wako. Shukrani kwa kuchagua kuwa member wa group hili na wote tuna nia moja ya kuidumisha Tanzania yetu na kuchangia maendeleo...

  • Said Luzigy Viongoz wetu ndio chanzo cha
    Migogoro hususani wafanyakazi wa ardhi ya handeni kwani huwa wanauza ardhi mara mbili na kukiuka maadili ya majukumu yao waliopewa na serikali.
  • Yasin Mohamed sina haraka nasubiri namsubiri Mhandeni sonyo afunguke kwanza
  • Kambi Mbwana Aha ha ha haaaaa. Kaka Yasin Mohamed, nimeona Mhandeni Sonyo ameandika kwa kupitia status ya jana. Labda hajaona hii mpya inayomuhusu piaa.
  • Kambi Mbwana Mhandeni SonyoNi sawa kabisa@Kambi. Maisha bora kwa kila Mtanzania na mwana Handeni inwezekana. Muhimu ni kama ulivyosema kilimo. Handeni tunategemea zao moja tu mahindi. Ikohaja ya kupata zao la biashara. Wakati wakoloni miaka ya 50 walijaribu zao la pamba hasa kule kwa Kwamsisi. Baada tu ya uhuru serikali ya TANU iliendrleza hili bila masanikio. Kwa ardhi na hali ya hewa wa Handeni mazao yanayofaaa Handeni zaidi ya mahindi ni maharage, kunde, pamba, alizeti, fiwi na tumbaku. Tuwe na mpango mkakati ambao katiks kilimo tuyaanngalie haya mazao na wapi yanastawi. Kisha ni muhimu maafisa kilimo wakatilia mkaxo kutembelra wskulima kuwaelekeza kilo bora kwa mazao ya chakula na biashara. Ni kweli kuna uhaba wa wstaalam lkn hao wachache tulionao watumike vizuri
  • Mhandeni Sonyo Ardhi ni rasilimali adhimu kwetu Handeni. Nashauri tuwe na mpango mkakati ambao pamoja na mengine utaonyesha ardhi yetu radilimali zake na sehemu za kilimo na udhibiti wake. Udhiniti ni muhimu tuweke kanuni za kuidhibiti ardhi yetu. Hivi sasa hakuna udhibiti viongozi wanauza ovyo ovyo ardhi yetu. Tunataka wajue sisi ndio wenyewe na takaekiuka tutalala nae mbele. Kuna ardhi ya madini mbunge na viongozi wengine wanapora na kuwauzia wageni kule magambazi wanalia ardhi kauziwa CANACO. Mazingara wanahaha kupata hati lakin wanaambiwa kuna kampuni 5 ndio zimepewa hiyo ardhi. Huko nyuma alitaka kuchukuq eka 10, 000 lakini mwenyekiti mahiri alitakaka ardhi hiyo ibaki kwa wananchi sasa hivi kwfanyiwa mizengwe ameachia. Bado wanahangaika. Kwachaga mpaka Kwankonje hali ni hiyo. Naambiwa ardhi kubwa kwediyamba, kwedizando, sasu mpaka nderema wandama inatakiwa na hao wakubwa. Tuulizie haya ama sivyo tutauzwa tukiwemo. Wageni wanauziwa ardhi yetu kama njugu. Nenda kwamgwe kwedizinga kwachaga kwankonje ndolwa kang'anta kote kuna ardhi imeuzwa na viongozi kwa njaa zao. Kuna kesi za wafugaji kuvamia maeneo ya kilomo bado zilo lkn hao viongozi wakihongwa pesa au ng'ombe kesi zinazimwa. Sehemu za konje misima kesi zipo. Kwa hiyo swala la ardhi ni mtambuka na lazima wilaya ije na mpango wa kudhibiti ardhi ama sivyo watoto wetu na vizazi vijavyo watakuja kuwa wageni kwenye nchi yao. Mwalimu alishaonya kuhusu hili tukiwaachia wachache wenye pesa kuhodhi ardhi ni hatari kwetu
  • Mhandeni Sonyo Migogorro mingi Handeni inatokana n viongozi wa kata na vijiji wanuza bila kufuata taratibu kwa ajili ya njaa na manufaa yao. Tuanzie hapo. Pia kuna viongozi wa wilaya nao wapo wachache wamejiingiza. Kuna wengine akiwemo mbunge wanchukua ardhi yenye madini na kuwauzia wageni. Ardhi nyingine imevamiwa na wafugaji wageni. Tuwe na mpango wa kupima vijiji na ardhi zao na kupewa hati. Pili tuwe na mpango mkakakati Handeni utakao ainisha ardhi ya kilimo, madini nk n kanunivza kuidhibiti ili iweze kuchangia maendeleo ya Handeni. Mbona Arusha, Mwanza Kahama Geita wanafaidika na madini yao. Tuwe na viongozi wanaoweka Handeni I mbele sio matumbo yao
  • Yasin Mohamed Naamini mi viongozi watakapo jiepusha na rushwa na ufisadi migogoro ya ardhi itapungua kwa asilimia kubwa.viongozi wafuate maadili ya kazi zao, wajiepushe kutoa eneo moja kwa mtu zaidi ya mmoja.
  • Yasin Mohamed serikali ihakikishe maeneo yote yamepimwa na pia iweke wazi maeneo ya malisho na maeneo ya killimo ili kuepusha migogoro baiba ya wakulima na wafugaji
  • Kambi Mbwana Kiukweli kabisa, migogoro ya ardhi ni tatizo Handeni na Tanzania kwa ujumla. Hata mkutano wa kujadiliwa kwa wanaotaka ardhi zaidi ya heka 50 pia halifuatwi. Wanafoji tu. Kuna siku zogo kubwa litaibuka. Shukrani mchangiaji mkuu, Mhandeni Sonyo kwa hoja..
  • Sanura Ali Naunga mkono wachangiaji karibu wote hili tatizo la ardhi ni limekuwa sugu mikoa karibu yote ya tanzania kilio ni ardhi.waziri aliyepewa dhamani angemaliza tatizo kwakuwa ni mjuzi.lakini bado watu wanauwana .wakulima na wafugaji.tukirudi handeni wenyekiti wa vijiji wanawauzia wageni waekari kwa maekari. Baada ya muda mfupi handeni ardhi yote watamiliki wageni.
  • Sanura Ali Hatukatai wageni ila ningeshauri mgeni auuziwe ila ipangwe isizidi labda eka kadhaa. Wananchi waelimishwe.kuhusu faida na hasara za kuuza ardhi.
  • Kambi Mbwana Ardhi siku hizi inauzwa kama njugu katika maeneo mengi ya Tanzania, hususan Handeni. Mtu ananunua ardhi kiurahisi kuliko hata anavyonunua suti dukani. Hili ni balaa kabisa. Tunaomba tuwe makini kwa wananchi na viongozi wa serikali za vijiji. Hili ni janga karibia kata zote Handeni.
  • Oumar Obs Bin Sebo Kikubwa ktk umilikaj wa ardh na nadhan ni sheria ya ardh izngatiwe vngnevyo migogoro itakuwa endelevu.. hata ktk uuzaj na ununuaj pia tuangalie haya maeneo tunauza ya nn na je vzaz vyetu vtakuja kumilik nn au tunataka kuwaandalia ukimbiz wa ndni ya maeneo yao waliozaliwa.
  • Kambi Mbwana Na hao wa kuzingatia sera na sheria za wardhi, yani viongozi wa vijiji na kata ndio wabangaizaji wanaotegemea ardhi. Mbaya hii jamani kama Oumar Obs Bin Sebo..
  • Mzigua Mzigua HAPA ktk migogoro ya ardh nadhani kila mtu anatambua thamani ya ardh na uhaba wa ardh ktk baadh ya mikoa imepekekea watu watafute popote inapopatkana.ukijumlisha na umaskini wa wananch wa wilaya ya HANDENI wanakubali kushawishika na kuwauzia mabosi wakgeni
  • Mzigua Mzigua Kingne ni viongoz wetu wanatumia ardh ya wananch kwa kivuli cha vyeo vyao na kujimilikisha ardh kinyume cha sheria wananch wanakosa pa kupeleka kilio chao cunajua HAKIMU FISI MBUZI hana sheria, bac mwananch anakua mnyonge hadi anashndwa kuvumilia.
  • Mzigua Mzigua JAMANI pia rushwa miongon mwa viongozi wa selikali pia viongoz wetu ni kama "MAPANYA" Wanang'ata kwa mkulima wanapulza kw WAFUGAJI. nadhan mfugaj anapsa kliko mkulim wanapew rushw n WAFUGAJI ndo mn hawafuatilii kero z wakulima "cz mkono mtupu haulambwi"..
  • Mzigua Mzigua naomba viongoz wetu wawajbike wafanye kazi kwa kufuata sheria nazani hii ndo itatufanya tushnd vita dhd ya migogoro ya ardh kinachowakera wakulima ni ongezeko la mifugo na ulishaji holela wa mifugo usiozingatia thamani ya mkulima na ardh yake..
  • Kambi Mbwana Mzigua Mzigua, unaeleweka vizuri sana.
  • Mzigua Mzigua nyie ni wa handeni lakini mimi ni wa handeni vijijini na mpaka sasa nacoment niko huku huku handeni tena vijijini na niko ktk kata ya kwamatuku ya mheshimiwa diwani BEREKO pia ni kata moja wapo yenye migogoro ya ardh iliyoshndkana

    INANIUMA SANA NDO MANA..
  • Yusuph Chabai Kwa kweli tatizo na migogoro ya ardhi ktk Tanzania yetu na wilaya zake ni sugu Tangu tangu na tangu,na mnyonge kudhulumiwa hilo ndilo jawabu,utakuta mtu ardhi karithi kutoka enzi ya mababu zake anaibuka mtu from no where anakuja na madocuments anadai yy ndio mmiliki wabwanga nyue hangi chahitahi,na ajabu hizo documenti amepata hukuhuko serekalini hapo ndo mapigano yanapoanza wenzetu wamakonde wanasema hapo chacha simchezo,ila wazigula wagamba msango ukomile tate kuzimu chose chiyuko
  • Kambi Mbwana Umesema kweli tupu kaka Yusuph Chabai, juu ya sekeseke hilo. Ndio maana nasema, wakati mwingine viongozi wa vijiji na wataalamu kutoka serikalini ni tatizo. Pia vipi mbinu ya kupima ardhi zote vijijini na kuwapatia hati wamiliki ili kuepusha zogo linaloendelea kutokea katika kaya mbalimbali. Kama naona linaweza kuwa na ufumbuzi. Kwa mfano, Kata ya Kwamatuku, kijiji cha Komsala na Kwamatuku wana mgogoro mkubwa wa ardhi. Mgogoro huu una miaka sasa. Na hakuna juhudi zozote zinazofanyiwa kazi. Nakumbuka hili suala liliandikwa pia gazetini,kuelezea jinsi lilipofikia.Kwakweli hali ni mbaya sana juu ya mgogoro wa ardhi Handeni na Tanzania kwa ujumla.
  • Yusuph Chabai Nimesikia kua kuna mpango mzuuri umeandaliwa huko kwabaya juu ya umiliki wa ardhi mzawa anapewa kipao mbele,na bei nafuu sipendi kuitaja,nimepata habari hizo kutoaka kwa Francis Mandevu,au mzungu,hilo ni jambo jema kabisa kuwapa kipao mbele wazawa juu ya umiliki wa ardhi,na wapa hongera saana wenzetu wa kwabaya,kwani wazigula wagamba alongole kalongola.
  • Kambi Mbwana “KATIKA nchi kama yetu, ambayo Waafrika ni masikini na wageni ni matajiri, kuna uwezekano mkubwa kwamba Mwafrika akiruhusiwa kuiuza ardhi, katika miaka themanini au miaka ijayo, ardhi yote ya Tanganyika itamilikiwa na matajiri wageni, na wenyeji watakuwa watwana.

    “Lakini hata kama wageni wasingekuwa matajiri, litaibuka tabaka la Watanganyika matajiri wajanja. Tukiruhusu ardhi iuzwe kama kanzu, katika muda mchache, kutakuwa na kundi dogo la Waafrika wakiwa na ardhi na walio wengi watakuwa watwana.”

    Mwl J.K. Nyerere, 1958. Kauli hii ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itaendelea kukumbukwa na Watanzania wote katika suala zima la ardhi.
  • Mzigua Mzigua KAKA YUSUPH CHABAI, hayo ni maneno au maandish yaliowekwa kwenye mafail gharama za uchapaj co sawa na rushwa watakayopewa kutkana na kummilikisha mmang'at heka 100. wtapta pesa watkula kuku watavimba vitambi af vinafunika makaratas yenye sera upo kaka ...
  • Yusuph Chabai Ila wenzetu wa wilaya ya Handeni zile sehemu muhimu za kitega uchumi tusekuzitaga,nakumbuka enzi nasoma Chanika primary school maeneo yoote ya hapo Handeni mjini yalikua yanamilikiwa na wazawa ni skanda peke yake na samji waliokua mjini kilichotokea hapo ni gharika la uuzaji maeneo uliovuka mipaka tukawapa wageni maeneo yoote muhimu ya biashara,sasa tupo kisongoni,nani aje kununua hidhaa,na ndio maana mzunguko wa pesa.wilayani kwetu ni mdogo mwenyenacho anacho asiekua nacho ndio hivyo tena,jamani ardhi ni mali lazima tuilinde,kwani ni kitega uchumi pia
  • Mzigua Mzigua dawa ya tatzo hili ni umaskini ulokithir unaopelekea mwananch wa handeni auze ardh alolithishwa na babu yake ili atatue matatzo yanayomkabiri nadhani selikali ilete siraha ambazo zitamfanya ashnde vita zid ya umaskini HAPO HATA UZA ARDH YA BABU YAKE...
  • Sanura Ali Kaka mzigua mzigua ndio maana nasisitiza kila kijana aliyopo nyumbani mwenye uwezo ,na mwenye uchungu na handeni agombee nafasi ya uongozi iwe diwani.mwenyeki ,katibu kata ili mradi kila nyanja ikae mtu makini matatizo yatapungua.sababu idara karibu zote zimekaa watu ambao wanathamini matumbo yao tu,mimi naimani tutaweza na tubadilike.
  • Sanura Ali Kwanza kaka mzigua mzigua chukuwa form ya udiwani .tupo pamoja mbona tunaweza?sema tunapenda jirudisha nyuma.mbona unaweza.tuache hii tabia ya kuogopa watu.hakuna aliyezaliwa kiongozi,wala hakuna shule ya kusomea,udiwani,n.k
  • Mzigua Mzigua uko sahihi dada sanura unajua huk uswz tunaogopana n pia tunatisha kw imani z kishirikina et kijan ukingia ktk ugombea unaingia ktk vita baina y wazee wny uchu w madaraka.
    ila nashukulu vjana wng wnamwmko ktk baadh y vjj ila kl kwny uzigua zaid wak fofofo
  • Sanura Ali Kaka mashaka muhando yupo wapi?maana kuna siku alikuja na sera nzuri ya ardhi ,tunahitaji kumsikia.
  • Sanura Ali Hiyo tabia ndio tuipige vita.hakuna kuogopo kurogwa tumezaliwa siku moja na utakufa siku moja ,muhimu kumuomba mungu wako tu.haiwezekani mtu yupo madarakani hana analolifanya,kazi yao fitina tu.
  • Mhandeni Sonyo Tupende Handeni yetu. Sote tunatoka sehemu mbali mbali huko. Tukubaliane kila mmoja wetu alipigie kelele swala hili la uuzaji kwa viongozi wa vitongoji vijiji na kata. Kwa wilayani tupiganie mkakati wa kudhibiti na kulinda ardhi yetu lakini tukipiga kelele kutoka Dar, Tanga, Arusha, Morogoro, Dodoma nk haitakuwa na tija. Ni kweli sasa hivi ukienda kwetu wageni waliouziwa ardhi hawatuthamini. Turudishe hadhi yetu kwa kuwa na viongozi waipendao Handeni. Wanaonunua uongozi kwa pesa ni wachimia tumbo na hawatajali maendeleo yetu. Chigambe haluse basi ama sivyo umasikini hautatuacha Handeni. Ushahidi si upo kwani Magambazi kauza nani?
  • Mhandeni Sonyo Naikumbuka kuisoma na hivi karibuni imerudiwa. Tusipokuwa makina watatokea wachache wenye pesa wakanunua ardhi na kuihodhi na kuwanyima wananchi wengi wa kawaida haki yai ns hivyo kuunda taifa la watu masikini na wachache matajiri. Tuwe makini hili lisiendelee Handeni. Tuidhbiti ardhi yetu kungali mapema.
  • Mzigua Mzigua unajua ntaingia kwny siasa ila kuna ubinafsi ktk vyma Vya siAsa wanpomgundua kijan hy ana sera y ukomboz utakaoperekea siri zao kufichuka hua wanambania sn kw sababu zsizo kua n kichwa wla miguu ILA VIJANA WANATKA KUFANY MABADLIKO YA UONGOZI HANDENI......
  • Mhandeni Sonyo Hiyo ni taarifa nzuri mgosi@Chabai. Lkn bado ni sehemu moja hii ingekuwa wilaya yote. Bado Kwamgwe, Kabuku, Kwamsisi, , Mkata nk wageni wsmehodhi maelfu ya hekta. Ni kweli katika nchi yetu una haki ya kwenda kuishi popote ila kwa Handeni akipata mmoja mgeni anawaita wengine hivyo kuhatarisha uwiano wa umiliki wa rasilimali na wenzetu Kilindi ni hivyo hivyo ingawaje huko walishapigana na wamasai lkn waarusha wapo wengi tu na wanazidi kuitana. Lengo sio kuwafukuza lkn wenye wilaya wawe na sauri kubwa
  • Mhandeni Sonyo Mashaka hana sera yoyote kwa Handeni. Yeye anapewa na mhe. Cha kuandika.. afadhali wenzetu Kilo, Mzigua, Kingama, Kambi, Masukuzi nk tuliangalie
  • Mhandeni Sonyo Na wewe mwenyewe Sanura. Kwenye nia ipo njia
  • Mhandeni Sonyo Tusiwe waoga. Mababu zetu wslitishwa na wakoloni Wajerumani, Waarabu, Waingereza. Sisi tupo nchi huru hakuna wa kuogopa ila tusivunje sheria. Tuna haki za msingi kudai chetu na kupanga tunayotaka. Hakuns aliyezaliwa na haki ya kuwa mbunge au diwani kama hafai out na tudhibiti rushwa na wixi wa kura. Kila kitu kinawezekana under the sun.
  • Mzigua Mzigua mwenzenu mi bdo mshamba hv ni kweli humu kwenye group kuna mtu anayetumiwa na huyu mheshimiwa? inamana anatuteka akili na kupeleka report sasa yeye haoni haja ya kuipigania wilaya yake?
    ILA TUSIINUE NAE GOGO MANA ATATUVUNJA MIGUU YY NI MNAFIKI TUMTENGENI-.
  • Mhandeni Sonyo Hakuna kuogopa kurogwa jamani Mwenyezi Mungu ndie Mlinzi mkuu
  • Mzigua Mzigua KAKA SONYO cc maendeleo tutayapata tutakapo fanya mabadiliko ya uongoz kuanzia mbunge ikiwezekana n chaMa kwasababu kura tulimpa kw ajir ya zile brauz alizotupa akirudisha gharama zke uchaguzi huo 2mtoe hatutafikia marengo ht kidogo MABADILIKO WANA HANDENI
  • Mhandeni Sonyo Kama alivyosema Kambi suluhisho ni kuwa na mkakati wa kupima ardhi ya vijiji na kupata hati miliki na sheria zisimamiwe. Zipo sheria tena nzuri
  • Mhandeni Sonyo Kama alivyosema Kambi suluhisho ni kuwa na mkakati wa kupima ardhi ya vijiji na kupata hati miliki na sheria zisimamiwe. Zipo sheria tena nzuri
  • Mhandeni Sonyo Hapo @Mzigua haswa. Matatizo ya wafugaji na wakulima yanaongezwa na rushwa ya wafugaji kwa viongozi waliopewa jukumu la kutafutia ufumbuzi. Ni kubwa na tulitafutie jibu. Mara nyingi wafugaji hada hawa wageni hutumia rushwa na sio Handeni tu sehemu nyingi
  • Mhandeni Sonyo Ni kweli viongozi wetu wengi wanakiuka sheria makusudi kwa manufaa yao. Huu ni uvinjaji wa sheria tuhakikishe wanawajibika
  • Mzigua Mzigua cc hatuwezi kuwawajibisha hatuna uwezo na nguvu uongozi wenyewe wa mabeberu hatuna afya tutaendelea kuonewa viongozi wetu hawaoni umuhimu wetu wanatuona mapundu kuwabeba tuwabebe kutuchapa watuchape jamani samani yetu kwenye kampeni 2 2kwapa kura wanasepa.
  • Sanura Ali Kaka zangu mhandeni sonyo na mzigua mzigua nawaona mpo juu kama dege la kivita,madiwani watarajiwa.safi sana.tupo pamoja
  • Mzigua Mzigua KAMA SISI MADIWANI WATARAJIWA WEWE MBUNGE MTARAJIWA, au hutaki kuwakomboa wazigua wenzio?
  • Sanura Ali Safi sana.uzalendo muhimu tupo pamoja wakuu.
  • Kambi Mbwana Baada ya wiki ya jana mdahalo wa maji kuchapishwa kwenye blog yetu ya Handeni Kwetu, www.handenikwetu.blogspot.com, huu nao utachapwa Jumatano ijayo kuwapa fursa watu kuyapitia mawazo ya wachangiaji wote. Kama unavyojua, wanaopitia blog ni wengi sana. Zaidi ya watu 200000 wanapitia, hivyo mawazo yetu yatasomwa na wengi sana... Tuendelee kuchangia mada na midahalo makini kama hii. Mzigua Mzigua umeingia kwa kasi sana. Muda wote ulikuwa wapi wapi? Safi sana...
    handenikwetu.blogspot.com
  • Mzigua Mzigua shukrani za zat kwa allah mana yy ndo amenijaria afy, sitomsahau mama yangu FATUMA RASHID OMAR MSONDE na baba yngu KAJEMBE HEMED MASUD wao ndo wamenizaa group member wote ambao wamesoma kile nilichoandika na kuchangia katika mjadala wa leo.
  • Mzigua Mzigua shukrani nyingene ziende kwa wale wajamaa wafupi weny macho madogo akina...SANCH,HUNCH NA HUNGJING PIA DONG FENG NA HUNG JING TAU mana wao wamekaa chn wameumiza kupata hk kisimu cha bei rahis kilichonifanya niwe sawa na wenye pesa

    TUKO PAMOJA WADAU .....

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...