Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa
klabu ya Simba, umesema kwamba kufanya vibaya katika mechi zake za Ligi Kuu
hakutokani na timu hiyo kutoandaliwa vizuri, isipokuwa ni hali ya mchezo wa
soka wenye matokeo ya kufungwa na kushinda.
Simba kwa
sasa inajiandaa na mechi yake dhidi ya Coastal Union, itakayopigwa Machi 23,
katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni baada ya kuahirishwa
baada ya kupangwa kufanyika leo.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema timu
yao imekuwa ikiandaliwa vizuri, lakini wanashindwa kupata matokeo mazuri ndani
ya uwanja.
Alisema hali
hiyo inasababishwa na ushindani uliopo kwenye ligi, hivyo ni wakati wa
mashabiki kutochukizwa na suala hilo.
“Tunashindwa
kupata matokeo mazuri uwanjani si kwasababu timu yetu haiandaliwi vyema kama
wanavyosema baadhi yao.
“Hivyo
tutaendelea na maandalizi yetu, tukiamini kuwa mechi ijayo dhidi ya Coastal
Union, hapo Machi 23 baada ya kusogezwa mbele,” alisema.
Simba
imeshindwa kuonyesha dhamira ya kunyakua taji msimu huu wa ligi, hivyo kuwapa
wakati mgumu mashabiki wao.
No comments:
Post a Comment