Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KLABU ya
Simba, imepigwa faini ya Sh Milioni moja, baada ya
kuhusishwa na vitendo vya ushirikina katika mechi yao dhidi ya Mbeya City.
Mbali na
adhabu hiyo, pia mshambuliaji wao Hamis Tambwe, naye amelambwa faini ya Sh
500,000, akihusishwa na kuonyesha alama ya matusi katika mechi hiyo na Mbeya
City.
Taarifa kutoka Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kupitia msemaji wao, Boniface
Wambura, alisema kuwa adhabu hiyo imeamuliwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania
(TPLB), iliyokaa Jumapili ya wiki iliyopita kwa ajili ya kupitia mechi mbalimbali
za Ligi ya Tanzania Bara na daraja la kwanza.
Wambura
alisema kuwa Simba walifanya makosa mbalimbali, hasa vitendo vinavyoashiria
ushirikina uwanjani, hivyo kuilazimu Bodi ya ligi iwapige faini.
“Simba walifanya
vitendo hivyo katika mechi yake dhidi ya Mbeya City ambapo imepigwa faini ya Sh.
500,000, pamoja na Sh. 500,000 nyingine kwa makocha wake Loga, Selemani Matola
na Idd Pazi kwa kudaiwa kuingia kumzonga mwamuzi katika mechi hiyo.
“Naye
mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe amepigwa faini ya Sh. 500,000 kwa
kushangilia bao alilofunga kwenye mechi hiyo kwa kuonesha ishara ya matusi kwa
kidole,” alisema.
Mbali na
Simba, Mbeya City nao walipigwa faini ya Sh. 300,000 kwa washabiki wake kuingia
uwanjani kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa mjini Bukoba, wakati Coastal
Union nao walipigwa faini ya kiasi kama hicho kutokana na mashabiki wao kurusha
chupa za maji uwanjani.
Wengine
waliotozwa faini ni kiungo wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi Sh 500,000, Salvatory Ntebe Sh 500,000, Musa Mgosi Sh 500,000,
Coastal Union Sh 500,000, JKT Ruvu Sh 300,000.
Kwa
upande wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) klabu zilizopigwa faini ni Friends
Rangers (sh. 200,000), Lipuli (sh. 200,000), Majimaji (sh. 400,000), Polisi
Morogoro (sh. 400,000) na Transit Camp (sh. 200,000).
No comments:
Post a Comment