Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, amesisitiza
umuhimu wa jamii kuweka mkazo katika kuibua vipaji kwa ajili ya maendeleo ya
vijana na wanaoshiriki katika sekta ya michezo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, DC Rweyemamu, pichani, alisema kuwa vipaji ni muhimu kuendelezwa kwa maendeleo ya Tanzania kwa ujumla.
Alisema hali hiyo inamfanya aweke mipango ya kuanzisha
mashindano mbalimbali, hasa yanayoshirikisha vijana wadogo kwa kuwakuza
kimichezo.
“Hii ni changamoto na dhamira ya kila mmoja wetu kufanya
juhudi za kuendeleza vipaji vya vijana wetu kwa ajili ya kuwapatia mwanga
mzuri.
“Hii ndio sababu tunajaribu kuwaza namna ya kuhakikisha
watoto wote wanaanza kucheza tangu wakiwa katika shule za msingi,” alisema.
Kwa mujibu wa DC Rweyemamu, anajipanga kuanzisha mashindano
ya vijana wadogo kwa ajili ya kuwakuza katika minajiri ya kuboresha vipaji
vyao.
No comments:
Post a Comment