https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, January 06, 2013

Chadema waja na mpya 2013


Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene wa pili kutoka kushoto, akifafanua jambo linalohusu chama chao.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimetangaza kuwachunguza na kuwapa ushauri wapenzi wao wanaoamua kufungua blogs na kuziita jina la (Chadema Blog), ili wajiendeshe bila kukiathiri chama chao.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene, alipokuwa akizungumza na Handeni Kwetu jana, kufuatia habari za baadhi ya blogs zinazojiita Chadema, taarifa zao kupingana kutokana na kuchukua stori kwenye baadhi ya magazeti.

Makene alisema sio blogs zote zinatumiwa na kuangaliwa na Chadema, hivyo ili wapenzi wao wajiendeshe vizuri, wataanza kuwapa somo, ikiwamo kuwazuia kuchukua stori zinazoandikwa katika magazeti mbalimbali nchini.

Alisema hawawezi kuwazuia watu hao, maana wanafanya hivyo kwa mapenzi ya kueneza sera za chama chao, lakini wakati mwingine wanashindwa kuelewa mbinu za kuandikwa habari hata zile ambazo zinalengo la kuhujumu chama chao.

Zimekuwapo blogs nyingi kama njia ya kupeana habari kwa mtandao, hivyo sisi Chadema tunashukuru kwanza kwa kupata Watanzania wengi wanaona kuwa wakifanya hivyo wataonyesha mapenzi yao kwa chama chetu hapa Tanzania.

Kwa sababu hiyo, tutakachofanya ni kuwaelimisha na kuwaambia kuwa sio kila habari inayotoka kwenye gazeti ni nzuri kwa Chadema, ukizingatia kuwa katika siasa kuna mbinu nyingi zinazotumiwa na vyama, hivyo hili litawasaidia kwa kiasi kikubwa,” alisema Makene.

Kwa mujibu wa Makene, habari zinazoandkwa na baadhi ya magazeti wakati mwingine ni za kupishana kiasi ambacho kinaweza kuwafanya wapenzi na wanachama wao washindwe kuelewa, ingawa aliwapongeza watu wote wenye mapenzi mema na Chadema hadi kufiia kuanzisha blogs kwa ajili ya kueneza elimu ya chama chao.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...