https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, January 17, 2013

Super D kumpika Idd Mnyeke kimasumbwi


Iddy Mnyeke kushoto akichuana na Mussa Sunga, katika mazoezi.

Na Mwandishi Wetu Ilala
BONDIA Iddy Mnyeke yupo katika maandalizi mazito ya kujiandaa na mpambano wake na Sadiki Momba utakaofanyika Februari 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam

Bondia huyo kwa sasa ananolewa na kocha wa kimataifa wa Mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo wameweka kambi ili kumkabili Momba

Akizungumza maandalizi ya bondia wake, Super D alisema amemwingiza kambini ili aweze kumtengeneza vizuri kwa ajili ya pambano lake.

Pambano hilo litakuwa la utangulizi kabla ya Deo Njiku na Omary Ramadhani kutwangana kugombea Ubingwa wa Taifa wa PST.
 
“Katika mpambano huo tutasambaza pia DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH.

“DVD za sasa zimeandaliwa vizuri na zikiwa na mchanganyiko wa aina yake katika ulimwengu wa masumbwi,” alisema.

DVD hizo huchanganya wakali mbalimbali, akiwamo Manny Pacquio, Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wengine akiwamo mkufunzi na bondia wa zamani, Habibu Kinyogoli.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...