https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, January 19, 2013

Yanga yawatandika Black Leopards 3-2 Taifa


Kikosi cha Yanga

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MABINGWA wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga SC, leo imewaangushia kipigo cha mbwa mwizi wageni wao, timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini, baada ya kuwatandika mabao 3-2.

Mabao ya Yanga yalipatikana katika dakika ya 32 lililowekwa kimiani kwa njia ya penati na Jerryson Tegete, Frank Domayo dakika ya 63, kabla ya 72 Tegete alipoongeza kalamu ya mabao kwa kuandika bao la tatu.

Mabao ya Black Leopards yalipatikana katika dakika ya 46 lililofungwa na Hampherey Khoza, huku lile la pili likifungwa na Rodney Ramagaleki katika dakika ya 88, hivyo matokeo kuwa bao 3-2.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani wa aina yake, kutokana na timu zote mbili kukamiana kwa ajili ya kuipatia ushindi, ila Yanga wao walikuwa juu zaidi na kufanikiwa kuibuka na ushindi huo mnono.

Mchezo huo ni wa Kimataifa wa kirafiki uliowakutani katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ukiwa ni mchezo mahususi kwa ajili ya kuwapima wachezaji wa Jangwani waliokuwa kambi ya wiki mbili nchini Uturuki.

Pia mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kwa timu ya Yanga inayojiandaa na mzunguuko wa pili wa Ligi ya Tanzania Bara, huku wao wakiwa kileleni.


No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...