https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, January 27, 2013

Mtanzania Onesmo Ngowi kucheza ndondi Afrika Kusini



 Ngowi akiwa na mwamuzi Jaap Van Niewenhuizen wa Afrika ya Kusini.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
RAIS wa IBF katika Bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Onesmo Ngowi, atasimamia pambano la ubingwa wa Dunia la vijana katika jiji la Johannesburg nchini Afrika ya Kusini, Februari 15, kati ya Mkongo, Illunga Mukaba atakayekipiga na Gogita Gorgiladze wa nchini Georgia. 
 
Katika taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari, Mabondia hao wenye wiwango vinavyolingana Georgita (12) na Makaba (12) watapambana kugombea mkanda wa vijana wa wa Dunia (Youth Title) wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika uzito wa Cruiserweight tarehe 15 February, 2013.

Mpambano wa wawili hawa utafanyika katika hoteli ya nyota 5 ya Emperors Palace in Kempton Park, Gauteng katika jiji la Johannesburg, nchini South Africa.

Ngowi kama kamishna mkuu wa pambano hilo atasaidiwa na maofisa wafuatao: Refarii: Wally Snowball (Afrika Kusini). Jaji Namba moja: Simon Xamlashe (Afrika Kusini), Jaji namba mbili: Manuel Maritxalar (Spain) na Jaji namba tatu: Jaap Van Niewenhuizen (Afrika ya Kusini). 
Mpambano huu ni kati ya mapambano zaidi ya 100 ya IBF yatakayofanyika katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika kipindi cha mwaka huu wa 2013 chini ya mradi wa IBF wa Utali wa Michezo.



No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...