https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, January 15, 2013

Wambura ajitosa Makamu wa Rais wa TFF



Michael Wambura, akisisitiza jambo.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa zamani wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa miguu (FAT), sasa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Michael Wambura, leo amechukua fomu za kuwania nafasi ya Makamu wa Rais, katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.

Wambura alichukua fomu jana za kuwania nafasi hiyo katika Ofisi za TFF, ambapo pia aliwaambia waandishi wa habari kuwa lengo lake ni kuchangia maendeleo ya mpira wa miguu, baada ya kipindi cha Leodgar Tenga kumalizika.

Wambura ameingia kwenye uchaguzi huo, huku akiwa na kumbukumbu ya kufanyiwa mizengwe, ambapo hata hivyo mwenyewe alikiri kukubali yaliyofanywa na Rais anayemaliza muda wake, Leodgar Tenga.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Wambura alisema,“Nimeamua kuchukua fomu kwa ajili ya kusaidiana na wadau wengine wa michezo kukuza na kuendeleza mazuri yaliyofanywa katika kipindi cha Tenga, ambaye hapana shaka ametangazaa kuwa hataendelea kugombea,” alisema.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema kuwa mbali na Wambura, wengine sita wamechukua fomu za kuwania ujumbe hivyo, hivyo kufikisha watu 27 waliochukua fomu hizo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...