https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, January 12, 2013

Kanisa latishwa na njaa Handeni


Mchungaji William Mwamalanga

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya Maadili ya Viongozi wa Dini, ambaye pia Mchungaji wa Kanisa la Pentekost, mkoani Mbeya, William Mwamalanga, amesema hali ni mbaya wilayani Handeni mkoani Tanga, kufuatia njaa na ukosefu maji safi na salama.

Akizungumza na Handeni Kwetu jana jijini Dar es Salaam, Mwamalanga, alisema kwamba njaa ni kali kiasi kwamba watu wengine wanakula maembe na mboga mboga.

Alisema baada ya kusikia hali hiyo kwenye vyombo vya habari, akiwa kama kiongozi wa dini, alilazimika kufunga safari hadi katika wilaya hiyo ili kuangalia balaa hilo.

“Hali ni mbaya, hivyo naomba wadau sasa waingilie kati kwa kunusuru watu ambao watapoteza utu na uhai wao kwasababu ya njaa, ambayo ndio tishio kubwa kwa wakazi wa Handeni.

“Nimetoka Mbeya kwa ajili ya kwenda Handeni na kukaa kwa wiki mbili nikitembelea sehemu kubwa ya wilaya, hivyo nimejionea mwenyewe na watu wajuwe hali si nzuri,” alisema Mwamalanga.

Hata hivyo serikali kwa kupitia Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa, walitangaza kupelekewa chakula cha bei rahisi, ambapo wananchi wao watalazimika kununua kwa bei isiyozi 750 hadi 900.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...