https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, January 10, 2013

CCM wataka michezo ipewe kipaumbele


 Yusuphed Mhandeni, pichani
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MCHUMI wa Kata ya Makumbusho wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Shaban, maarufu kama (Yusuphed Mhandeni), amewataka viongozi na wadau kuweka mkazo kwenye suala la michezo, maana linaweza kuleta maendeleo.

Yusuphed aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mipango ya kuwazindua watendaji hasa wa kwenye kata yao ili wawekeze kwenye michezo na kuwapa fursa vijana kuonyesha uwezo wao uwanjani.

Akizungumza zaidi, Yusuphed ambaye pia ni kada wa CCM katika Kata ya Makumbusho, alisema kwa kuangalia fani ya michezo, ukiwamo mpira wa miguu, ngumi na mingineyo, vijana wao watapata ajira.

Alisema hali hiyo inasababisha mkazo kuwekwa humo, hasa kwa viongozi ambao wana nafasi na sababu zote za kuwapatia watu wao ajira kwa kupitia michezo.

"Sisi wote kwa pamoja tukiwekeza kwenye michezo, ajira zitakuwa nyingi, hivyo nadhani watendaji na viongozi kwa pamoja waliangalie hilo.

"Kwa mfano kata ya Makumbusho ina vijana wengi na wenye uwezo wa kuingia kwa wingi kwenye michezo, hivyo watu wajuwe wajibu wao," alisema Yusuphed.

Mbali na kupenda michezo, Yusuphed ni miongoni mwa wadau muhimu wa muziki, huku akijitolea kusaidia kwa karibu watu waliokuwa kwenye sanaa hiyo, wakiwamo wanamuziki.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...