https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, January 21, 2013

Azam yaonyesha matumaini Kenya, kucheza kesho na KCB


Na Mwandishi Wetu, Kenya
BAO pekee la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba wa Azam FC, limeipa ushindi timu hiyo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya SOFAPAKA uliochezwa jana Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya.

Azam FC imecheza mchezo wake wa pili wa kirafiki, juzi jioni walifungwa 2-1 na AFC Leopard katika mechi iliyochezwa uwanja huo.

Katika mchezo huo, kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoka suluhu, wachezaji wa Azam FC Himid Mao alipiga mpira wa adhabu uliogonga mwamba na kurudi ndani katika dakika ya 14, dk 22 Seif Abdalah akiwa na lango la SOFAPAKA alipiga mpira uliotoka nje.

Azam FC waliendelea kufanya amshambulizi katika lango la SOFAPAKA, dk 27 na 45 Michael Bolou alipiga shuti likatoka nje na dakika ya 37 Humprey Mieno alishindwa kufunga na badala yake shuti likaokolewa na kipa wa SOFAPAKA, Duncan Ochieng
SOFAPAKA dk 24 Kago Dawson alikosa nafasi ya wazi kwa kupiga shuti lililodakwa vyema na kipa chipukizi wa Azam FC, Aishi Salum ambaye aliweza kulinda lango hilo katika vipindi vyote.

Kipindi cha pili Azam FC walifanya mabadiliko walitoka Samih Haji Nuhu, Michael Bolou, Khamis Mcha na David Mwantika nafasi zao zikachukuliwa Luckson Kakolaki, Abdulhalim Humud, Gaudence Mwaikimba na Malika Ndeule,mabadiliko hayo yaliimarisha kikosi hicho na kufanya mashambulizi mengi.

Kipa Aishi Salum alitumia vema nafasi aliyoipata katika mchezo huo kwa kuzuia mashuti ya wachezaji wa SOFAPAKA na kusimama vema katika nafasi hiyo, kutokana na umri wake mdogo amecheza katika kiwango cha juu kama anavyokuwa golikipa namba moja Mwadini Ally ambaye jana alipumzishwa na kuwapisha vijana Aishi na Jackson Wandwi.
Azam FC walipata goli katika dakika ya 58 kupitia kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na Mwaikimba baada ya beki wa SOFAPAKA Kisuya Colins kunawa mpira katika eneo la hatari.

Goli hilo lilidumu hadi kumalizika kwa mchezo huo na kuifanya Azam FC kushinda 1-0 katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Raisi wa SOFAPAKA, Elly Kalekwa na Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrissa.
Azam FC kesho itapumzika na kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa City ambao watacheza siku ya Jumanne dhidi ya KCB na kumalizia safari hiyo ya mechi za kirafiki ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya ligi kuu na Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Azam FC, Aishi Salum, Himid Mao/Omary Mtaki, Samih Haji Nuhu/Luckson Kakolaki, Jockins Atudo, David Mwantika/Malika Ndeule 45’, Michael Bolou/Abdulhalim Humud 45’, Humphrey Mieno/Ibrahim Mwaipopo 66’, Salum Abibakar, Brian Umony Jabir Aziz 81’, Seif Abdalah/Uhuru seleman 68’, Khamis Mcha/ Gaudence Mwaikimba.

SOFAPAKA  Duncan Ochieng/Okeko David, Shivash Collins, Kisuya Collins, Situma James, Felly Mulumba, Abdalah Nyanzi, Hilary Echesa, Koko Manopi, Kagogo Patrick/George Owino, Kago Dawson na John Baraza/Tarumbwa Cabadian.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...