https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, January 14, 2013

Mbabe wa Maoja kumvaa Ankrah wa Ghana



 Gottlieb Ndokosho akinyanyua mkanda wake

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA Gottlieb Ndokosho kutoka nchini Namibia aliyemchapa kwa KO bondia Rajabu Maoja wa Tanzania, atapanda tena uliongoni Februari 2 mwaka huu katika jiji la Windhoek, nchini Namibia kupambana na bondia Prosper Ankrah kutoka nchini Ghana.
 
Wawili hao watapambana katika mpambano wa mwaka wakati Ndokosho wakati atakapotetea mkanda wa IBF wa bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika uzito wa unyoya. Ndokosho aliupata mkanda huo tarehe 29 Septemba 2012 wakati alipomshinda Mtanzania Rajabu Maoja katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa SPK jijini Windhoek, nchini Namibia.

Akizungumzia mpambano huo, Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kimataifa Afrika (IBF) na  Ghuba ya Uajemi, Onesmo Ngowi, alisema pambano lingine Namibia litawakutanisha mabondia Albinus Felesianu wa Namibia atakapopambana na bondia Asamoah Wilson kutoka nchini Ghana katika uzito wa Super Featherweight.

Wakati huo huo bondia mkali wa Tunisia Ayoub Nefzi mwenye makao yake nchini Belgium atapambana na bondia Ishmael Tetteh wa Ghana kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG)

Bondia anayekuja juu kwa kasi wa Ghana Richard Commey atachuana na Mgahana mwenzake Bilal Mohammed kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.

Mpambano huu utafanyika sambamba na ule utakaowakutanisha Mtanzania Fadhili Majia na Isaac Quaye wa Ghana. Mtanzania mwingine Allen Kamote atapimana nguvu na bondia machachari na bingwa wa WBA wa mabara Emmanuel Tagoe wa Ghana siku hiyo hiyo tarehe 22 Februari.

Naye bondia mwana dada Helen Joseph wa Nigeria atapambana na bondia Mariana Gulyas wa Hungary kugombea mkanda wa IBF wa mabara katika uzito wa Unyoya. Mpambano wa wanadada hao utafanyika katika jiji la Accra, nchini Ghana tarehe 30 mwezi wa March, 2013.

Hili litakuwa pambano la kwanza kwa bondia Helen Joseph tangu apoteze pambano la IBF la ubingwa wa dunia nchini Dominican Republic alipokutana na bondia Dahianna Santana wa Domoinican Republic.

Mapambano hayo yote yatasimamiwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...