https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Wednesday, January 16, 2013

Yusuf Manji ajitosa uchaguzi wa TFFYusuf Manji kushoto, akipewa fomu na mmiliki wa timu ya African Lyon, Rahim Zamunda.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Yusuf Manji, ameingia kwenye mbio za uongozi za Shirikisho la Soka nchini (TFF), baada ya kuchukuliwa fomu na mmiliki wa klabu ya African Lyon, Rahim Zamunda leo katika ofisi za TFF.

Manji akizungumza na waandishi wa habari.

Zamunda alimchukulia fomu za kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu kwa nia ya klabu za Ligi Kuu zilizompendekeza mwenyekiti huyo wa Yanga.

Uchaguzi huo utafanyika Februari 24 huku ukizidi kuleta msisimko wa aina yake kutokana na majina ya wanamichezo wanaojitokeza katika patashika hiyo.

Mbali na Manji, wengineo waliochukua fomu leo ni pamoja na Jamal Malinzi, Athumani Nyamlani na Omari Mussa Nkwarulo, ambao wamechukua fomu za kugombea urais wa TFF.

Uchaguzi wa TFF unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka hapa nchini, ikiwa ni hatua ya kupatikana viongozi wapya, hasa baada ya kipindi cha rais anayemaliza muda wake, Leodgar Tenga kumalizika na kutangaza kutogombea tena nafasi hiyo.


No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...