https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, January 15, 2013

Vifungashio vyamuumiza kichwa mjasiriamali



Elizabeth Kilili, Mkurugenzi Grace Products Ltd

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MJASIRIAMALI na mzalishaji wa bidhaa mbalimbali kutoka Grace Products Ltd, Elizabeth Kilili, amesema kwamba changamoto anazokutana nazo sasa ni vifungashio ili bidhaa zake zionakane katika mwonekano mzuri zaidi.

Elizabeth aliyasema hayo jana alipokuwa anazungumza na Handeni Kwetu, ikiwa ni tamko lake la kwanza katika kipindi cha mwaka mpya wa 2013.

Alisema mipango yake kwa sasa ni kuhakikisha kuwa bidhaa zake, ikiwamo lotion yake Gurlic and lotion inakuwa nzuri zaidi kwa kuwa na kifungashio kizuri na kinachoficha mafuta hayo.

“Kama unataka kufanya biashara kimataifa zaidi, lazima nihakikishe kuwa bidhaa zangu zinakuwa nzuri kuanzia vifungashio vyake na bidhaa yenyewe kwa ujumla.

“Naamini mambo yatasaidia kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wa Tanzania tunasonga mbele zaidi kwa kuhakikisha kuwa tunakabiriana na vikwazo vyotee,” alisema Elizabeth.

Mwanamama huyo ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Grace Products Ltd, ameingiza sokoni bidhaa nne, yakiwamo mafuta ya kupaka, sabuni ya kuogea ya Grace Manjano, Shampooo ambazo zote kwa pamoja zipo chini ya kampuni yake.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...