https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, January 08, 2013

Wafanyabiashara wa Tanzania kuula Ujerumani



Onesmo Ngowi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati limewaalika wafanyabishara wa Tanzania kuhudhuria mkutano wa mwaka wa IBF/USBA utakaofanyika katika jiji la Berlin nchini Ujerumani kuanzia Mei 21-25 mwaka huu.
 
Katika mkutano huo wanachama zaidi ya 3000 wa IBF/USBA kutoka nchi zaidi ya 200 duniani watahudhuria.
 
Taarifa iliyotumwa na Rais wa IBF Bara la Afrika na Ghuba ya Uajemi, Onesmo Ngowi, ilisema hiyo ni fursa pekee kwa wafanyabishara wa Kitanzania kuweza kutumia mkutano huo kutangaza biashara zao katika sekta mbalimbali hususan sekta ya Kitalii, TEHAMA, usafirishaji wa bidhaa za Tanzania nje ya nchi pamoja na uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini.
 
Mkutano wa mwaka wa IBF/USBA huwakutanisha wafanyabishara waliowekeza katika sekta mbalimbaki za kiuchumi na hutoa fursa kubwa kwa wafanyabishara kujenga mitandao mzuri wa biashara.
   
Aidha, Ngowi anawahamasisha wakuzaji wa mchezo wa ngumi pamoja na wale wanaofanya shughuli za Branding (kukuza biashara) kuhudhuria mkutano huu na kujipatia fursa mbalimbali za biashara.
 
Ngowi ataongoza ujumbe nzito kutoka bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati wakiwamo Mawaziri wa Michezo kadhaa kutoka nchi zilizo katika ukanda huu.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...