https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, January 18, 2013

Yanga kuwaonyesha kazi Black Leopards kesho

Wachezaji wa timu ya Black Leopards wakitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, tayari kuwavaa Yanga kesho.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MABINGWA wa zamani wa Tanzania Bara, Yanga SC, kesho inaingia uwanjani kumenyana na Black Leopards ya Afrika Kusini, ambao tayari wameshatua nchini leo.
Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni na maandalizi yake yamekwisha kamilika huku waandaaji wakipunguza viingilio ili kuwawezesha mashabiki wengi kufika.
Mratibu wa mechi hiyo, Shafii Dauda wa Prime Time promotion alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na wamepunguza kiingilio cha Sh 5,000 na Sh 7,000 na kuwa cha Sh 3,500 ili mashabiki wengi waingie kuangalia mchezo huo wa Kimataifa wa kirafiki.
Viingilio vingine ni shs 7,000 kwa viti vya rangi ya machungwa, wakati VIP C ni Shs 15,000, VIP B Sh 20,000 na VIP A Sh 30,000.
Kocha wa timu hiyo, Abel Makhubela alisema kuwa wanauzoefu wa siku nyingi na walifanya ziara nchi mbali mbali katika afrika na kuja Tanzania ni moja ya faraja kwao.
Ziara hii ziara yetu ya kwanza Tanzania, tumefanya ziara nchini Zimbabwe na nchi nyingie, tulipata matokeo mazuri na vile vile tunatarajia kupata matokeo mazuri hapa, nimekuja na wachezaji wangu wote wa kikosa cha kwanza, jumla ya wachezaji ni 23, mashabiki watarajie mchezo mzuri,” alisema Makhubela.
Alisema kuwa wanaijua Yanga na Simba ni moja ya timu nzuri na maarufu bara la Afrika na hivyo wamejiandaa kwani ni kipimo kizuri cha ligi ya kwao ambayo ipo katikati.



No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...