https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, January 12, 2013

Yanga kurejea Tanzania Jumatatu


Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako

Na Mwandishi Wetu, Uturuki
TIMU ya Yanga, inatarajia kuondoka nchini Uturuki kesho mchana
baada ya kumaliza kambi yao ya wiki mbili waliyoweka nchini kwa
ajili ya kujiandaa na ligi ya Tanzania Bara, hatua ya mzunguuko
wa pili.

Ligi hiyo imepangwa kuendelea tena baadaye mwezi huu, huku timu
mbalimbali zikijiandaa kwa ajili ya kufanya vizuri katika
patashika hiyo.

Yanga inarejea Tanzania, huku ikiwa na kumbukumbu ya kumaliza
vibaya mechi zao za Kimataifa za kirafiki, baada ya kukubali
kichapo cha bao 2-0 dhidi ya Emmen FC inayoshiriki ligi daraja
la kwanza nchini Uholanzi.

Mechi hiyo ya mwisho ilichezwa katika Uwanja wa Arcuda Football uliopo Antalya, huku ikileta huzuni kwa wachezaji na mashabiki wa Yanga.

Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, amesema kuwa Yanga baada ya kuondoka mchana wa siku ya Jumapili ya Januari 13, itaingia jijini Dar es Salaam alfajiri ya siku ya Jumatatu.

Kufuatia kipigo hicho cha bao 2-0, kocha wa Yanga, Ernest Brandts, aliumizwa na matokeo huku akisema timu yake ilicheza vizuri, ingawa walishindwa kuwa makini zaidi na kufungwa mabao hayo.

Kwa mujibu wa Kizuguto, Yanga inayofanya mazoezi ya mwisho leo mchana nchini hapa, itaanza safari ya kurudi Tanzania siku ya jumapili mchana, ambapo itafika Dar es salaam alfajiri ya siku ya Jumatatu.

Kikosi kilichoanza kipindi cha kwanza: Said Mohamed, Juma Abdul,
Stephano Mwasika,  Nadir Haroub 'Cannavaro', Shadrack Nsajigwa,
Nurdin Bakari, Saimon Msuva, Frank Domayo, Geroge Banda, Nizar
Khalfani,  Haruna Niyonzima.

Kikosi cha kipindi cha pili: Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar
Joshua, Ladislaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd 'Chuji,
Godfrey Taita, Omega Seme, Didier Kavumbagu, Jerson
Tegete/Rehani Kibingu, David Luhende.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...