https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, January 29, 2013

Nyosh: Sijamroga mwimbaji wangu Ngwasuma



Rais wa FM Academia, Nyosh el Sadaat

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
RAIS wa bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ Nyosh El Sadaat, amekanusha uvumi ulionea hapa nchi kuwa ndiye aliyemroga mwimbaji Alpha Kabeza.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Nyosh alisema hawezi kufanya kitu kama hicho na anashangazwa na taarifa hizo.

“Mimi sijui ni kwanini wanasema hivyo, ila sijamroga Kabeza na kwanini nimroge, niko Ngwasuma tangu zamani, yeye amekuja mwaka 2006, sasa namroga ili iweje?,” alisema Nyosh.

Kabeza, ambaye mwanzoni aliondolewa kwenye bendi ya Ngwasuma kutokana na kuwa msumbufu, amekuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kwa muda sasa, huku baadhi ya mashabiki wakidai kuwa amerogwa na Nyosh, kutoka na uwezo wake wa kuimba vizuri.

Bendi hiyo wiki hii itaendelea na ratiba zake kama kawaida, ambapo Jumatano watakuwa New Maisha Club, Jumamosi watapiga Ukumbi wa Kijiji cha Makumbushi na Jumapili kumaliza kwa bonanza kwenye Ukumbi wa New Msasani Club.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...