https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, January 26, 2013

Vurugu Mtwara, nyumba ya mbunge yachomwa moto


Anna Abdallah, Mbunge wa Viti Maalum na Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HALI inaendelea kuwa mbaya mkoani Mtwara, baada ya baadhi ya wananchi kufanya vitendo visivyokuwa vya kiungwana kwa kuchoma moto na kuharibu mali mbalimbali, kwa madai kuwa madereva wa bodaboda wanaonewa katika shughuli zao.

Leo tayari wananchi hao wamechoma moto nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho, sambamba na kuchoma ofisi ya Halmashauri, Ofisi ya CCM na vitu vingine, ikiwa ni muendelezo wa kadhia hizo mkoani Mtwara.

Wakati hayo yakiendelea, jana katika mkoa huo pia kuliwa na tatizo kama hilo, baada ya nyumba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia.

Habari kutoka kwa mtu aliyekuwa mkoani Mtwara zinasema kwa ujumla wananchi wengi wamekumbwa na taharuki kufuatia harakati hizo zilizopamba moto, hasa chanzo chake kikiwa gesi, ingawa jana kuliibuka tena sakata la ushirikina, kwa madai kuwa nyumba ya diwaniwa Kata ya Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mohamed Chehako kuwa inahifadhi wachawi.

Sakata hilo lililazimisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliovamia nyumba hiyo.

Juhudi za kupata matukio yanayoendelea mkoani Mtwara leo zinaendelea, ikiwa ni pamoja na kuendelea kuchambua kwa undani sakata hilo linalokolea kila siku ya Mungu, hivyo kuweza kuwagawa wananchi.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...