https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, January 29, 2013

Mganga aliyekwapua dawa Kilindi akamatwa





Mkuu wa Wilaya Kilindi, Selemani Liwowa.



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MGANGA Mkuu wa Zahanati ya Saunyi, wilayani Kilindi, Rashidi Mhande, amekamatwa na polisi, ikiwa ni agizo la Mkuu wa wilaya hiyo, Selemani Liwowa, baada ya kuiba dawa.

Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita katika zahanati hiyo, ambayo mganga huyo aliiba dawa zenye thamani ya Sh Milioni tano na kukimbia kusipojulikana.

Akizungumza na Handeni Kwetu muda mchache uliopita, Liwowa alisema Mhande amekamatwa, baada ya kutafutwa kwa siku kadhaa.

Alisema baada ya mganga huyo kukimbia, aliagiza atafutwe ili sheria zifuate mkondo wake, endapo atakutwa na hatia katika sakata hilo la wizi wa dawa.

“Mara baada ya kupata taarifa za wizi huo na yeye kukamatwa, niliagiza kuwa asakwe popote alipokimbilia, hasa baada ya kufanikiwa kuondoka hospitali ya wilaya, alipotibiwa kwa kudanganya kuwa alipigwa na wananchi jamii ya wafugaji wilayani hapa.

“Nashukuru sasa amekamatwa, hivyo taarifa zaidi zitatoka na kitakachofuata juu ya tukio la kuiba dawa lililofanywa na Mhande, kama Mganga Mkuu wa zahanati hiyo,” alisema Liwowa, DC wa Kilindi.

Kukamatwa kwa Mganga huyo ni tukio jema kwa maendeleo ya watu wa Kilindi, hasa kwa kuzingatia kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakifanya vitendo vya uhujumi uchumi.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...