https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, January 08, 2013

Njaa yatikisa wilayani Kilindi

Na Mwandishi Wetu, Kilindi
MKUU wa Wilaya ya Kilindi, pichani, Selemani Liwowa, ametangaza njaa katika wilaya yake na kutaja kata zilizoathiriwa zaidi kuwa ni pamoja na Saunyi, Kwediboma, Mkindi, Jaira na Kisangasa.

Akizungumza na Handeni Kwetu leo asubuhi wilayani hapa, Liwowa alisema tayari wameshaomba chakula kutoka kwenye mfuko wa hifadhi wa chakula (NFRA), wakiomba kupewa tani 70,000.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kilichosababisha njaa katika eneo wilaya yao ni kutokana na watu kuuza chakula chao mapema, huku wakishindwa kujiwekea akiba katika kaya zao.

Alisema jambo hilo ni baya, huku wakitarajia chakula hicho kitakachapolekwa kuuzwa kwa bei isiyozidi 750 hadi 900, wakati bei iliyopo sasa ni 1200 hadi 1300 na kuwafanya watu waishi kwa tabu.

“Tumeshafanya utaratibu wa kuwasiliana na wenzetu wakiwamo NRFA ili watuletee chakula cha bei rahisi kwa ajili ya watu walioathiriwa na njaa hii katika wilaya yangu ya Kilindi.

“Naamini chakula kitakapofika wananchi wetu watakipata kwa bei rahisi, maana masharti ni kwamba watu wachangie kidogo kwa bei yaa 750 au 900,” alisema Liwowa, Mkuu wa wilaya Kilindi.

Mbali na Kilindi, wilaya ya Handeni nayo imekumbwa na baa la njaa, baada ya Mkuu wake wa wilaya, Muhingo Rweyemamu naye kuomba msaada kwa ajili ya kuwanusuru baadhi ya wananchi wake wilayani humo, ambazo zote kwa pamoja zinaunda Mkoa wa Tanga, unaongozwa na Chiku Gallawa.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...