Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akiongoza mapokezi ya ujumbe
wa Sekretarieti
ya CCM,unaoelekea mkoani Kigoma mapema asubuhi hii kwa usafiri wa
treni,ukiongozwa na Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (wa pili
kulia) kwenye
maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM yatakayo adhmishwa mkoani
humo.
Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.
Asha-Rose Migiro akiwa ndani ya treni asubuhi hii akiwapungia
mkono WanaCCM wa Mkoani Dodoma waliofika kuwalaki na kuwatakia safari
njema Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa
treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akishuka
katika treni Mjini Dodoma

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akizungumza na Wanachama wa CCM mkoani Dodoma waliokuwa wamefika
Stesheni ya Dodoma asubuhi hii kuwalaki Wajumbe wa Sekretarieti ya
CCM wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka
36 ya chama cha Mapinduzi CCM. Wajumbe waliondoka jana ni Katibu wa NEC, Siasa na
Mahusiano ya Kimataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro na kulia kwake ni Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM Nape
Nnauye.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg.
Abdulrahman Kinana akiagana na baadhi ya WanaCCM wa Mkoani Dodoma waliofika
kuwalaki na kuwatakia safari njema Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, wanaoelekea mkoani
Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha
Mapinduzi CCM,Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka jana jijini Dar kwenda
Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.

No comments:
Post a Comment