https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, January 08, 2013

CCM Handeni yawapinga wawekezaji wa kukata mkaa


Na Mwandishi Wetu, Handeni
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Handeni, Athumani Malunda, pichani, amewataka wananchi kuwakataa wawekezaji wanaoingia wilayani humo kwa kisingizio cha kuchukua mashamba kwa ajili ya kilimo lakini badala yake, wanachoma mkaa na kukata mbao na kuleta hatari ya jangwa wilayani humo.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kilimamzinga kilichopo kata ya Kang'ata wilayani hapa, Mwenyekiti huyo alisema wawekezaji wa aina hiyo hawafai hata kidogo.

“Ndugu zangu wa Kilimamzinga, hawa mliotueleza kwamba wameweka mnara wa simu na leo hii wamewapa fedha za kujengea nyumba ya mwalimu wanafaa sana sababu wanatusaidia katika maendeleo yetu.

“Ila tusikubali kupokea wawekezaji wanokuja kwa lengo la kutaka mashamba ili walime lakini baadaye wanachoma mkaa na kupasua mbao, tutakosa mvua wilaya yetu tukizidi kukata miti," alisema Malunda.

Mbunge wa jimbo hilo, Abdallah Kigoda, akizungumza katika mkutano huo amewataka viongozi wa kata kuligawa haraka shamba la mwekezaji huyo katika kijiji hicho cha Gole kwa kuwa taratibu za kupewa mwekezaji huyo zimekiukwa.

Pia ametaka viongozi wa kata kufanya utafiti katika maeneo mengine katika wilaya hiyo mashamba ambao yamekiukwa utaratibu wapewe wananchi wa Handeni ambao wengi wao hawama mashamba ya kutosha.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...