https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, January 21, 2013

Wacheza filamu wapanga kumtingisha rais Kikwete



Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
HALI inazidi kuwa mbaya kwa vurugu na maandamano, baada ya wasanii kutangaza kufanya maandamano mfululizo, endapo Serikali itaendelea kuchekea dhuluma na manyanyaso wanayoendelea kufanyiwa wasanii hapa nchini.
Michael Sangu, Mwenyekiti TDFAA

Hatari hiyo ilitangazwa jana na wasanii zaidi ya 200 waliokutana katika Ukumbi wa Vijana, Kinondoni, wakiongozwa na viongozi wao kutoka Mashirikisho mbalimbali, ikiwamo lile la Filamu TAFF.
Simon Mwapagata, msanii wa filamu Tanzania

Handeni Kwetu ilikuwapo katika viwanja hivyo na kukuta wasanii wengi waliokuwa wakijadili mambo yao huku wakiwa na hasira kali kutoka kwa viongozi, hasa wale wa COSOTA na Bodi ya Filamu Tanzania, chini ya Mkurugenzi wake, Joyce Fisoo.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania (TDFAA), Michael Sangu, alisema sheria zilizotungwa kwa ajili ya wasanii hazina mashiko.

Alisema sheria hizo zitazidi kuongeza maisha duni kwa wasanii Tanzania, kama walivyokufa baadhi yao wakiwa hawana chochote cha maana zaidi ya kufanikiwa kuwa maarufu.

“Mchakato mzima wa kanuni za utekelezaji wa sheria ya filamu na michezo ya kuigiza Tanzania Bara haukuhusisha wasanii wadau, wakiwamo wasanii.

“Hii ni hatari maana itaongeza ugumu wa utendaji kazi, huku wachache wao kuendelea kufanikiwa, huku serikali ikiwa kimya, jambo ambalo kwa pamoja hatiwezi kulichekea,” alisema.

Awali wasanii wengi walipata kutoa maoni yao katika kutafuta maisha bora ya wasanii, huku lawama zao zote wakizielekeza kwa watendaji wa juu wa COSOTA, chini ya Yustus Mkinga na Joyce Fisoo wakitaka waondoshwe katika nafasi zao.

“Kama hakutakuwa na mabadiliko katika nafasi za watu hawa, hakika hatuwezi kufanya nao kazi, maana kauli zao, matendo yao katika suala zima la sanaa hatuna imani nayo,” alisema Simon Mwapagata akiungwa mkono na mamia ya wasanii wenzake.

Endapo wasanii hao watafanya maandamano bila kuchoka kushinikiza watendaji hao wang’oke katika nafasi zao, ni wazi nao watakuwa wameingia katika kutingisha utawala wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, mmoja wa viongozi wa juu wan chi wanaokubaliwa na waliokuwa karibu mno na wasanii hapa nchini.

Serikali kwa kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inapaswa kuliangalia hilo kwa haraka kabla ya kuzidi kuingiza chokochoko katika vuguvu vugu hizo za wasanii kwa kusikiliza kilio cha wasanii wao.
 

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...