https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, January 26, 2013

Nani atamtambia mwenzake kati ya Mandulla na Martin kesho?


Bondia Antony Mathias (kushoto) akitunishiana misuri na Fadhili Majia baada ya kupima uzito, Dar es salaam  kwa ajili ya mpambo wao kesho utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Tandale.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA Hassan Mandulla na James Martin wanatarajia kupanda ulingoni kesho Jumapili, Januari 27 katika Ukumbi wa wa CCM Tandale, jiji Dar es salaam.

Muandaaji wa pambano hilo, Waziri Rosta, amesema mabondia hao wamepima uzito leo pamoja na kujua afya zao kwa ajili ya kivumbi hicho cha wanamasumbwi.

Mbali na mabondia hao, pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kama vile, Fadhili Majia, atakayekipiga na Anthon Mathias,
Kalama Nyilawila na Athumani Pendeza.
Michezo mingine ni Shabani Kilumbelumbe na Mwaite Juma, huku Charles Mashali akivaana na Adam Ngange, wakati Julius Noro akivaana na Abdallah Luwajempambano, Rajabu Tumaini na Daudi Anton, huku Rashid Mohamed akipigana na Eliman Richard, bila kusahau Rashid Hamisi atakayepigana na Omary Shabani.

Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.

Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.

“Katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition,” alisema.  

Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.   

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...