https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, January 16, 2013

Mpiganaji wa vita vya pili vya Dunia afariki Dunia



Marehemu Anthon Simbaulanga

Na Mwandishi Wetu, Handeni
MPIGANAJI wa Vita vya pili vya Dunia, Mzee Anthon Simbaulanga, amefariki Dunia jana, Januari 15, katika kijiji cha Komsala, wilayani Handeni mkoani Tanga, huku akihisiwa na kuwa na miaka isiyopungua 120.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Magunga, iliyopo wilayani Korogwe mkoani Tanga, huku akitarajiwa kuzikwa kesho katika makaburi ya kijiji cha Komsala.

Habari zilizoifikia Handeni Kwetu na kuthibitishwa na mtoto wa marehemu, Paulina Anthon Simbaulanga, zilisema mwili wa baba yao utazikwa kesho baada ya ndugu kuungana kwenye msiba huo mzito katika familia yao.

“Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Magunga kwa ajili ya kusubiri ndugu waliokuwa sehemu mbalimbali kuwasili kwa maziko yake,” alisema.

Mzee Simbaulanga, alipofanya mazungumzo na Handeni Kwetu mwishoni mwa mwaka jana, alionyeshwa kukerwa na kunyimwa haki yake ya mafao baada ya kupigana vita vya pili vya Dunia.

Habari za mafao yake zilifika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, wilayani Muhingo Rweyemamu na kuagiza kukutana na mwakilishi wa mzee huyo ili azungumze naye na kujua cha kufanya, ukizingatia kuwa ndio kwanza ameingia katika wilaya hiyo, baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete mwaka jana.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...