https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, January 19, 2013

Ramadhani Shauri kuzipiga na Said Njechele kesho Mabibo

Ramadhani Shauri akipima uzito
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa na Bingwa wa IBF Intercontinental, Ramadhani Shauri, anatarajiwa kupanda ulingoni Jumapili ya kesho kwa ajili ya kuzipiga na Said Njechele wa Iringa, katika pambano la kirafiki la raundi nane katika Ukumbi wa D.I.D Hall, uliopo Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam.
Ramadhani Shauri kulia akipimana ubavu na Said Njechele

Mratibu wa pambano hilo Charles Christopher,  amesema kuwa maaandalizi ya pambano hilo yamekamilika na mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani, sanjari na kupima uzito.
Ambapo pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi na mabondia watakaosindikiza pia wamepima chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim kamwe na docta john wapo sawa kwa kupambana.

Mabondia watakaocheza utangulizi ni Hamis Mohamed na Haruna Mnyalukolo, Pendeza Shomari akipizipiga na Martin Richard, wakati Mbaruku Nassoro akipanda ulingoni dhidi ya Karimu Respect, huku Doto Mustafa naye akipigana na Shomari Miurundi, bila kusahau Issa Omari, akipigana na Juma Kashinde.

Katibu Mkuu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe, amethibisha kuwa kanuni na taratibu za ngumi za kulipwa zimefuatwa na mabondia wapo katika hali nzuri ya kupigana kwenye pambano hilo.


No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...