https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, January 19, 2013

Bushoke kutambulishwa Sikinde kesho Jumapili


Maxmilian Bushoke akiwa na mtoto wake Bushoke nyuma.

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa siku nyingi nchini, Maxmilian Bushoke, anatarajia kutambulishwa rasmi katika kikosi cha wanamuziki wa bendi ya Orchestra Mlimani Park, baada ya kurejea nchini hivi karibuni na kujiunga na bendi hiyo.

Bushoke alikuwa akiimbia bendi hiyo tangu miaka ya kati ya 1980, kabla ya kuhamia nchini Afrika Kusini alikokuwa akifanya shughuli za utangazaji.

Akizungunza na Handeni Kwetu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa bendi hiyo, Jimmy Chika, alisema Bushoke atatambulishwa katika Ukumbi wa Pentagon, uliopo Kurasini ambapo pia atafanya shoo na wanamuziki wenzake kuanzia Jumapili ya Januari 20.

Mwimbaji huyo na mtunzi aliwahi kujizolea sifa baada ya kutunga nyimbo kama Kiu ya Jibu, Penzi kile cha fikara na nyingine kadhaa.

Bushoke ambaye ni baba mzazi wa msanii wa kizazi kipya, Luta Bushoke, amekuwa akijiunga na bendi hiyo mara kwa mara alipokuwa akirejea hapa nchini, ambapo hata hivyo sasa atakuwa na bendi hiyo kwa kipindi kirefu.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...