https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, January 16, 2013

Malinzi, Nyamlani kukabana koo Urais TFF

Jamal Malinzi, akisaini baada ya kurudisha fomu leo TFF

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Chama cha Soka mkoani Kagera (KRFA), Jamal Malinzi amekuwa wa kwanza kurudisha fomu za kuwania nafasi ya Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), katika Uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.

Jamal Malinzi akishuka kwenye gari lake leo TFF

Mbali na Malinzi, Makamu wa Rais, Athumani Nyamlani, naye alijitokeza katika uchukuaji wa fomu wa nafasi hiyo nyeti, ikiwa ni baada ya rais anayemaliza muda wake, Leodgar Tenga, kutangaza kujiweka kando kwenye uchaguzi huo.
Athumani Nyamlani kulia, akipokea fomu za kugombea nafasi ya Urais wa TFF

Akizungumza muda mfupi baada ya kurudisha fomu hiyo, Malinzi alisema kwamba anaamini muda wake wa kuwa rais wa TFF umefika kutokana na uzoefu mkubwa aliokuwa nao katika michezo.

Alisema mwaka 2008 alipogombea nafasi hiyo, kura zake hazikutosha, hivyo uvumilivu wake, uwezo wake katika masuala ya michezo, ukiwamo mpira wa miguu, mambo yatakuwa mazuri na kufanikiwa kuipata nafasi hiyo.

“Sitaki kusema maneno mengi kwasababu muda wa kampeni bado, hivyo lakufanya navuta subira huku nikiwataka wenye uwezo wa kuongoza wachukuwe fomu ili atafutwe mtu mmoja katika nafasi ya Urais wa TFF.

“TFF kumekuwa na utulivu wa aina yake hasa kutokana na sera nzuri za Tengaa, ambaye ametangaza kutogombea tena nafasi hii, hivyo wa kuvaa kiatu chake atapatikana baada ya uchaguzi huo kukamilika,” alisema.

Naye Nyamlani alisema kuwa TFF sio taasisi ya kujaribu kujifunza kuongoza, hivyo kwake yeye uwezo anao wa kuongoza kutokana na uzoefu aliokuwa nao baada ya kuwa Makamu kwa miaka minne.

“Nimeiva vizuri ili niwe rais wa TFF, hivyo baada ya kampeni kuanza nitatangaza sera na mikakati yangu, maana naamini kwa sasa muda wake bado zaidi ya kusubiri watu wengine wenye nia yao kugombea nafasi za uongozi wa TFF,” alisema.

Kinyang’anyiro hicho kimeibua joto kali kutokana na wanamichezo wengi kuhamasika katika uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za TFF.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...