https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, January 22, 2013

Hisia za hatari zaendelea kutishia sakata la gesi Mtwara



Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SERIKALI inapaswa kuliangalia kwa kina sakata la gesi mkoani Mtwara na Lindi, kutokana na chokochoko zinazoendelea kutolewa na wananchi wa mikoa hiyo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo

Wananchi hao, wamekuwa wakipigania gesi isitoke nje ya mkoa wao wa Mtwara, wakiwa na nia ya kuhudumia mkoa huo kwa madai kuwa hauna maendeleo kwa miaka 51 ya Uhuru.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Handeni Kwetu, walitangaza kuwa harakati zao hazitakoma hadi watakapoona serikali yao imesikiliza kilio chao.

“Na Tatizo la mikoa ya Kusini sio gesi bali ni kusahauliwa kwa miaka 51 ya Uhuru. Korosho, reli, Bandari, miundo mbinu, tatizo la elimu na kuwa waanga wa ukombozi wa nchi zilizopo kusini mwa Afrika.

Wanasiasa kujiingiza katika hoja si ajabu kwasababu duniani kote wanasiasa ndio huibua matatizo ya wananchi , maana wasomi wetu wengi hawana meno ya na ndio wanaopitisha  mikataba mibovu .

Sio choyo, lakini tunafikia wakati tunajuta kwa nini sisi Mtwara Lindi tumekuwa sehemu ya Tanzania. Tuna rasilimali tosha za kuweza kuitwa, kama vile Bandari, Bahari, Ardhi yenye rutuba, watu, mito, madini, korosho, ufuta, mhogo na nyinginezo.

Kusini tuna haki ya kumdai mume wetu Tanzania haki zetu za msingi, maana tumevumilia mno hadi kilio cha kwi kwi. Ni mimi mwanaharakati,” ulisema ujumbe huo uliotoka kwa mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Amoni, mwenye namba +255652221100.

Kwa habari zaidi juu ya sakata hili la gesi na maoni yaliyotumwa kutoka kwa wadau wa Mtwara na Lindi, usikose kusoma Makala ya Mgodi Unaotembea kesho Jumatano, Januari 23, katika blog yako ya Handeni Kwetu.

Katika makala hayo, mambo mbalimbali yamejadiliwa kwa kina, sambamba na kutoa fursa ya kutoa vilio vya wananchi hao waliotuma maoni yao kwa njia ya simu na barua pepe.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...