https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, January 21, 2013

Kipenga cha pingamizi chapulizwa uchaguzi TFF

Jamal Malinzi, mgombea Urais wa TFF

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), limebandika majina ya wagombea wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi za Shirikisho lao kwa ajili ya kuwapa fursa wadau wa michezo wawaone na kuweka pingamizi wanapoona wanafaa kwa kuafuata masharti ya kanuni za uchaguzi.



Michael Wambura, mgombea Makamu wa Rais TFF

Majina hayo yamebandikwa kwa kufuata kanuni za uchaguzi za TFF kwa mujibu wa ibara ya 11 (1), (2) na (3), ikiwa ni njia ya kuwafanya wanamichezo wengine kutoa fursa kwa wale wote wenye pingamizi kwa watu wasiopenda wagombee katika Uchaguzi huo wa TFF.

Athumani Nyamlani, kulia, mgombea urais TFF

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika vyombo vya sambamba na Handeni Kwetu Blog, ilisema pingamizi lolote litakalomuhusu mgombea yoyote, lazima liwe kwa maandishi.

Mbali na maandishi hayo, lieleze kwa uwazi sababu za pingamizi, liambatanishwe na ushahidi wa pingamizi, liwe na jina kamili la mtoa pingamizi, anwani ya kudumu na saini ya mwanamichezo huyo.

Wagombea waliobandikwa majina yao kwa ajili ya kuwekewa pingamizi ni pamoja na nafasi ya urais kwa Athumani Jumanne Nyamlani, Jamal Emily Malinzi na Omary Mussa Nkwarulo, huku nafasi ya Makamu wa Rais wakitajwa Michael Richard Wambura, Ramadhan Omar Nassib, Wallace Karia.

Wajumbe waliopitishwa ni Abdallah Hussein Mussa, Kalilo Samson, Salum Hamis Umande Chama, Jumbe Oddessa Magati, Mugisha Galibona, Samuel Nyala, Vedastus F.K Lufano, Epaphra Swai, Mbasha Matutu, Charles Mugondo, Elley Simon Mbise, Omary Walii Ali.

Wengine ni Ahmed Idd Mgoyi, Yusuf Hamis Kitumbo, Ayubu Nyaulingo, Blassy Mghube Kiondo, Nazarius A.M Kilungeja, Seleman Bandiho Kameya, David Samson Lugenge, Eliud Peter Mvella, John Exavery M. Kiteve, Lusekelo E. Mwanjala, James Patrick Mhagama, Stanley W. D Lugenge, Athuman Kingome Kambi, Francis Kumba  Ndulane, Zafarani Mzee Damoder na Hussein Zuberi Mwamba.

 Wagombea wengine ni Stewart Ernest Masima, Farid Nahdi, Hassan Othuman Hassan, Riziki Juma Majala, Twahil Twaha Njoki, Davis Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed, Kusianga Mohamed Kiata, Alex Crispine Kamuzelya, Juma Abbas Pinto, Muhsin Said Balhabou, Omary Isack Abdulkadir, Shafii Kajuna Dauda, huku Richard Julius Rukambura, akiondolewa kwa sababu ya kuvunja kanuni za uchaguzi, wakati Titus Osoro, akijitoa mwenyewe.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...