https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, January 20, 2013

Mkuu wa Mkoa Tanga ataka Kilindi watunze mazingira



 Mkuu wa Mkoa Tanga, Chiku Gallawa

Na Rahimu Kambi, Kilindi
MKUU wa Mkoa Tanga, Chiku Gallawa, amewataka Watanzania na wananchi wa wilayani Kilindi kuhakikisha kuwa wanatunza mazingira ili wapate maisha bora, hasa kwa kupitia kilimo.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa

Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na wananchi wa Lumutio, katika ziara yake ya siku nne inayomalizika leo wilayani hapa, kabla ya kuelekea jijini Tanga kuendelea na kazi zake nyingine za ujenzi wa Taifa.

Akizungumza zaidi, Chiku Gallawa alisema kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakifanya shughuli za ukataji wa mkaa bila kufuata sheria wala maagizo ya serikali yanayokataza kazi hizo.

Alisema watu hao wamesababisha hatari kubwa ya ukame na kuleta jangwa na ukosefu wa mvua katika baadhi ya maeneo kutokana na matatizo ya watu wachache, jambo ambalo haliwezi kufumbiwa macho.

“Hii haiwezi kuchekewa wala kufumbiwa macho na serikali, hivyo ni jambo la msingi kwa kila mwananchi wa wilayani Kilindi na Tanzania kwa ujumla kuhakikisha kuwa inatunza mazingira.

“Tukitunza mazingira, kuhifadhi misitu na miti yetu inayovamiwa kwa kasi na watu kwa ajili ya ukataji wa mkaa, hakutakuwa na jangwa wala badiliko lolote, hivyo kuwa tunu kwetu,”  alisema.

Ziara ya Mkuu huyo wa Mkoa Tanga, ilisimamiwa kwa umakini na mwenyeji wake, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwamo jingo la wazazi la zahanati wilayani humo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...