https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, October 27, 2013

Mwidau CUP yarindima Wilayani Pangani mkoani Tanga, huku ikitarajia kutumika zaidi ya mili 20


Na Mwandishi Wetu,Tanga

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau kupitia Chama cha Wananchi(CUF),  amezindua rasmi ligi ya Mwidau Cup inayoshirikisha timu 45 za Wilaya ya Pangani yenye kata 13 huku zaidi ya sh.milioni 20 zikitarajiwa kutumika hadi kumalika kwa ligi hiyo.
 Mbunge Amina Mwidau, akikagua timu huku akiwa na viongozi wa timu ya Black burn kabla ya mchezo kuanza.

Kwa mujibu wa Mwidau lengo la mashindano hayo si kupata tu mshindi kwa ajili ya kuchukua zawadi, bali anataka kuona vipaji vya soka vinaibuliwa kwa kuwa soka ni ajira na wakati huo huohuwaunganisha wananchi pamoja na hiyo ndio dhamira yake kwa Wilaya ya Pangani na Tanga kwa ujumla.
 Mbunge Amina Mwidau, akikagua timu huku akiwa na viongozi wa timu ya Black burn kabla ya mchezo kuanza.

Akizungumza katika Uwanja wa Kumba Wilayani Pangani wakati akizindua ligi hiyo, Mwidau alisisitiza umuhimu kwa timu ambazo zinashiriki kuonesha uwezo wao wa kusakata soka na  anatamani kuona Wilaya ya Pangani inakuwa chachu katika maendeleo ya soka kwa mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), akifutiliana kwa makini pambano la soko kati ya timu ya Black burn na Nondo (kulia), ni Katibu Msaidizi wa Chama cha Soko Wilaya ya Pangani, Mohamed Swazi, katika pambano hilo timu ya Black burn iliibuka na ushindi wa bao 4-1.


“Malengo yangu ni kuona tunapata vipaji vya soka kwa vijana wetu maana uwezo wanao. Hivyo nimeamua kuanza na Wilaya ya Pangani kwa kudhamini ligi hii nikiwa na maana ya kupata sehemu ya kuanzia katika kuhakikisha Mkoa wa Tanga unakuwa na ligi ya aina hii,”alisema.


Alifafanua yeye ni mdau mkubwa kwenye michezo na amekuwa akitoa vifaa vya michezo kwa timu za mpira wa miguu na mpira wa wanawake lakini ni wakati muafaka wa kudhamini ligi na ndio maana ameamua kutoa sh.milioni 20 kuona michezo inapewa nafasi kwa kuwa na mashinano ya Mwidau CUP.


Akizungumzia zaidi kuhusu ligi ya Mwidau Cup, alisema kuwa ametoa vifaa ya michezo kwa timu zote zinazoshiriki ligi hiyo na jumla ya thamani yake kuanzia vifaa na mambo mengine ya udhamini jumla ya sh.milioni 20 zitatumika lakini jambo la msingi kwake kuona michezo ndani ya mkoa huu inapewa kipaumbele.


Aliongeza kuwa yeye ni mbunge wa Mkoa wa Tanga , hivyo anayo fura ya kushirikiana na wadau wa michezo katika kuleta maendeleo na kuweka wazi historia inaonesha mkoa huo umekuwa maarufu katika michezo kutokana na wachezaji wengi maarufu kutoka mkoani hapa.


Hata hivyo alisisitiza nidhamu kwa vijana katika suala la michezo kwani, ndio njia pekee ya kufikia kwenye mafanikio na kwamba hata katika suala la maendeleo ili liweze kufanikiwa linahitaji nguvu ya wananchi kwa ujumla wao bila kujali itikadi za vyama vya siasa, hivyo mashindano hayo yatawaunganisha katika burudani lakini pia katika kufanya kazi kwa ushirikiano.


Mwidau , mbali ya kutoa vifaa vya michezo kwa timu za mpira wa miguu, pia alitumia nafasi hiyo kutoa vifaa vya michezo kwa timu ya mpira wa  Netball kwa Wilaya ya Pangani huku akisisitiza kuwa amefanya hivyo kwenye maeneo mengine ya mkoa wa Tanga.


Katibu Msaidizi wa Chama cha Soka Wilaya ya Pangani, Mohamed Swazi, alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa chachu kwa vijana kutumia muda mwingi kujihusisha na michezo huku akitumia nafasi hiyo kufafanua changamoto iliyopo kwenye timu yao timu nyingi hazina vifaa vya michezo, lakini kwa uamuzi wa mbunge wa Mwidau wanaamini wamepata mwanzo nzuri wa kuendeleza michezo kwa kasi.


Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Pangani Kemmy Anatori, alisema kuwa anatambua umuhimu wa michezo na kwa upande wake akiwa mwakilishi wa Serikali anaunga mkono juhudi za Mwidau za kuhamasisha michezo kwenye wilaya yake kwani faida ni nyingi kuliko hasara.

Kwa timu ambazo zimefungua pazia ya ligi hiyo, timu ya soka ya BlackBurn imefanikiwa kuibuka mshindi baada ya kuibamiza timu ya soka ya Nondo mabao 4-0.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...