https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Monday, October 07, 2013

Kaseba awapa somo wadau wa masumbwi Tanzania


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Japhet Kaseba, amewataka vijana kuzidi kuchangamkia fursa za mchezo huo kwa ajili ya kuonyesha vipaji vyao, sambamba na kukuza mchezo wa ngumi.
Japhet Kaseba, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema endapo vijana watazidi kujiingiza katika ngumi, harakati njema za kuuendeleza mchezo wa masumbwi zitashika kasi.

Alisema anaamini huo ndio mpango wenye mashiko katika ngumi, ukizingatia kuwa bila vijana makini na wenye uchu wa mafanikio, mambo yatakuwa magumu katika kushuhudia mafanikio ya ngumi.

“Kikubwa ni kuhakikisha kuwa vijana wanapata hamu zaidi ya kushiriki katika mchezo wa masumbwi kwa ajili ya kufanikisha ndoto zao sambamba na kuongeza ushindani kwa mabondia wote.

“Vijana wanapoingia katika masumbwi, kila bondia anapata mshindani wake, ukizingatia kuwa wale wanaofahamika hawawezi kubaki milele, hivyo lazima damu change zishike kasi,” alisema.

Kaseba ni miongoni mwa mabondia wenye mafanikio, huku akiwahi kuwa Bingwa wa Dunia wa Ngumi za mateke, ambapo mara kadhaa amekuwa akikosa mpinzani wa kupambana naye ulingoni.


No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...