https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, October 21, 2013

Msanii Stevu Nyerere kupakua filamu ya Long Time akiwa na wakali kibao chini ya Proin Promotions Ltd

Msanii Nguli wa Uigizaji wa filamu Tanzania Steven Megele almaarufu Steve Nyerere akielezea ujio wa nguvu wa filamu yake mpya iitwayo Long Time ambayo imetengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions wakati alipofanya mkutano na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo Katika Ofisi za Proin Promotions zilizopo Mtaa wa Ursino Jijini Dar.Filamu hiyo pia itasambazwa na kuuzwa na  Kampuni ya Proin Promotions Limited kupitia Mawakala wao Nchini Nzima kuanzia leo
Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Evans Stephen (wa Kwanza kulia) na Msanii Nguli wa Filamu Tanzania Steve Nyerere kwa pamoja wakionyesha ukurasa wa filamu mpya ya Proin Promotions  iitwayo long Time mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Proin Promotions zilizopo Mtaa wa Ursino Jijini Dar 
Steve Nyerere akiongelea ujio wa Nguvu wa Filamu yake mpya  iitwayo Long Time ambayo inaingia sokoni leo, Filamu ambayo imeigizwa kwa ustadi wa hali ya juu na kuwa na uhalisia wa maisha ya Mtanzania.
Meneja Masoko wa kampuni ya Proin Promotions Bw Evans Stephen akiongelea juu ya ujio wa nguvu wa filamu ya Long Time iliyoigizwa na Wasanii mahiri Steve Nyerere na Johari.Filamu hiyo imetengenezwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited na itasambazwa na kuuzwa na Mawakala Wa Proin Promotions Limited Nchini Nzima na itaanza kupatika leo katika Sehemu Mbalimbali za Tanzania.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Msanii wa Filamu Tanzania Steve Nyerere akiwa pamoja na Meneja masoko Wa Proin Promotions Bw Evans Stephen wakati wakiitambulisha filamu mpya kutoka Proin Promotions iitwayo Long Time
Mmoja wa waandishi wa Habari (katikati) akiuliza swali kwa mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Proin Promotions ambao ndio watengenezaji,wauzaji na wasambazaji wa Filamu yao Mpya iitwayo Long Time ambayo imeigizwa na Wasanii mahiri na nguli Steve Nyerere, Johari na wengine wengi .

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya utengenezaji,uuzaji na usambazi wa filamu za kitanzania Kutoka nchini Tanzania ya Proin Promotions leo imetambulisha rasmi filamu yake mpya iitwayo Long Time ambayo itapatikana kuanzia leo sokoni kwa gharama ya Shilingi Elfu tano tu za kitanzania

Filamu ya Long Time ni filamu ambayo imetengenezwa na kampuni mahiri ya Proin Promotions limited na kuigizwa na wasanii wakongwe na nguli wakiwemo Steve Nyerere, Blandina Chagula na wengine wengi.

Proin Promotions limited imejikita katika kubadilisha soko la filamu Tanzania na kuleta mapinduzi ya kweli katika tasnia ya filamu nchini,Na  takribani nakala laki moja za Filamu ya Long Time zishaingia soko leo na kuuzwa.

Long Time ni filamu ambayo inafundisha na kuburudisha na pia inayoelezea Uhalisia wa maisha ya Mtanzania.

Jinsi ya Kupata nakala yako ya Long Time unaweza kutembelea maduka yanayouzwa filamu za kitanzania na Kwa Mawakala Wote wa Proin Promotions Wanaopatikana Nchi Nzima Vilevile unaweza kuagiza oda yako ya filamu za Proin Promotions Limited kupitia tovuti yao ya www.proinpromotions.com na katika ukurasa wao wa facebook kwa kulike ukurasa huo bofya kiunganishi hiko https://www.facebook.com/proinpromotions.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...