https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, October 09, 2013

King Majuto: Njaa, shida za wananchi zinanilazimu nigombee Ubunge Tanga Mjini 2015


Na Kambi Mbwana, Dar es Salam
MSANII wa filamu na vichekesho wa muda mrefu hapa nchini, Amri Athuman maarufu kama King Majuto, amesema hali ya Tanga ilivyokuwa sasa na ugumu wa maisha unamlazimisha aingie kwenye siasa kwa ajili ya kuwania Ubunge mkoani Tanga.
Msanii wa vichekesho Tanzania, Amri Athuman, maarufu kama King Majuto, pichanii, aliuhakikishia mtandao huu nia yake ya kuwania Ubunge mwaka 2015 kwa tiketi ya CCM

Majuto anataka kugombea Ubunge katika Jimbo la Tanga mjini, ambapo kwa sasa lipo chini ya Mbunge wake Omar Nundu, jambo linaloanza kuibua maswali kede kede miongoni mwa wadau wa sanaa wanayempenda mzee Majuto.

Mbunge wa Tanga Mjini, Omar Nundu, pichani.
Akizungumza na Handeni Kwetu mapema wiki hii, King Majuto alisema kwamba atagombea Ubunge kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), chama anachokipenda na kukiheshimu kwa kiasi kikubwa mno kutokana na mfumo wake wa uongozi.

Alisema watu wamekuwa wakiishi maisha magumu na yenye kukatisha tamaa, hivyo ni wakati wake sasa kuingia katika ulingo huo ili amalizie wakati wake kwa ajili ya kuwapatia maisha mazuri wananchi wa Tanga na Tanzania kwa ujumla.

“Kuna watu wanaweza kusema labda njaa ndio inayonifanya niingie kwenye siasa na kutaka kuwania nafasi kubwa ya Ubunge, ila lazima wajuwe kuwa sina njaa kwakuwa kazi ninayoifanya inanipa fedha za kutosha na maisha yangu ni mazuri.

“Nina mpangilio mzuri wa kazi zangu, bado naheshimika kwa kiasi kikubwa na kazi zangu zinapendwa, ila kuingia kwenye siasa ni kwasababu nina malengo mazuri na wanananchi wa Tanga Mjini na Tanzania kwa ujumla, hivyo hakuna wa kunizuia,” alisema Mzee Majuto.

“Kwa sasa nipo sawa zaidi na malengo yangu hayo naoamba Mungu yafanikiwe bila kuogopa majina ya wanasiasa waliokuwapo au wanaoweza kupambana na mimi katika nafasi hiyo, tukianza ndani ya CCM na baadaye Uchaguzi Mkuu,” aliongeza Majuto.

Kauli ya King Majuto inaweza kuleta picha ya kupendeza kwa wadau wa sanaa Tanzania, huku akiwa ni miongoni mwa wasanii wanaokubalika kwa kiasi kikubwa mno. Bila shaka kwa kauli hiyo inaongeza ugumu wa siasa za mwaka 2015 huku kila mmoja akiona ana uwezo wa kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa hapa Tanzania.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...