https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Monday, October 07, 2013

Wamiliki wa malori waendelea kuwasha moto kwa serikali Tanzania


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania, TATOA, Zakaria Hans Pope, amesema kwamba  mara kadhaa serikali imeshindwa kutambua na kusikiliza vilio vyao, hasa mpango mpya wa kukamata magari yatakayoegeshwa barabarani.
Akizungumza mapema leo asubuhi na kituo cha radio cha Capital Radio, Hans Pope alisema mpango huo hauna lengo jema kwao.
Malori yakiwa yamepaki.
“Tumeweza kuzungumza mara kwa mara na viongozi wa serikali lakini hakuna kinachosikilizwa ingawa katika vikao hivyo tunafikia muafaka na kudai watarekebisha.

“Yapo mambo mengi ambayo kwa kawaida yanachochea mazingira magumu ya utendaji kazi wa magari ya kubeba mizigo na kuna kila sababu ya kuliangalia suala hili kwa ajili ya kuondoa utata,” alisema.

Mvutano mkali umeibuka kwa siku mbili hizi kutokana na madereva wa malori kuanza kuweka mgomo hali inayosababisha pia mwingiliano mkubwa katika barabara hapa nchini, hususan katika mizani.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...