https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, October 05, 2013

Serikali yajigamba kufikisha huduma za TEHAMA hadi vijijini

Na Magreth Kinabo, MAELEZO
SERIKALI imesema kwamba   inatarajia kuboresha   Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kila kijiji ili  huduma zake ziweze kuwa karibu na wananchi ili kusaidia kupunguza gharama wanazozitumia.
 Picha na 1
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwasili katika ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao zilizopo jengo la TTCL mtaa wa Samora leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia shughuli za usimamizi wa mifumo na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika uendeshaji wa shughuli za serikali Picha na 2
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na viongozi wa Wakala ya Serikali Mtandao na waandishi wa habari  leo jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea taarifa  kuhusu maendeleo ya Tovuti Kuu mpya ya serikali inayosimamiwa na Wakala ya Serikali Mtandao chini ya Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma. Balozi Sefue amefafanua kuwa Tovuti Kuu ya Serikali iliyoanzishwa itawawezesha wananchi kupata taarifa na huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali.


Aidha  Serikali  imeeleza  kwamba iteendelea kujenga uwezo wa  kiufundi wa   kuweza kuzuia  uvujaji wa siri, uhalifu na udhibiti wa sheria ndani ya  vyombo vyake ili taarifa za siri zisiweze kuvuja.

 Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi  Ombeni Sefue  wakati alipotembelea  ofisi ya  Wakala  ya Serikali Mtandao(e GA) jijini Dares Salaam kwa ajili ya kuzungumza na menejimenti na wafanyakazi.

“Leo nimetembelea ofisi hii. Ni eneo la kipaumbele kwa Serikali   kwa kuongeza matumizi   ya TEHAMA kwa Serikali, tija, kasi ya utendaji kazi na huduma za Serikali. Hivyo sehemu hii ni muhimu ya kuifanya Serikali iwe karibu na wananchi. Tovuti hii iwe ni dirisha   la mwananchi kutatuliwa shida yake.,”alisema huku akitoa wito kwa wananchi wawe tayari kuitumia.

 Balozi Sefue  alisema tatizo la changamoto  la TEHAMA   kuhusu  uvujaji wa siri  lipo dunia nzima hata Marekani  wanakabiliana  nalo ,hivyo  ufumbuzi wake si kuachana nalo bali kuzuia uvujaji huo na uhalifu kwa kujenga uwezo wa udhibiti.

“Lazima kuwe na udhibiti mfano wa kisheria  tayari tunayo sheria  tutaendelea kuiboresha kulingana na changamaoto zitakazo kuja,” alisisitiza Balozi Sefue.

 Alisema kupitia TEHAMA wananchi wataweza kupata matibabu au elimu  na kulizia huduma wanazotakiwa kuzipta mfano miradi ya visima vya maji imefikia hatua  zipi.

Aliongeza kuwa hivi sasa wakala huo unaandaa mifumo ya kuwezesha Wizara, Idara na taasisi mbalimbali za Serikali kufanya kazi kwa ushirikiano.

Akizungumzia  kuhusu ufikishaji wa huduma katika maeneo ya vijijini, Mtendaji Mkuu wa (eGA) Dk. Jabiri Bakari alisema watatumia ubunifu ili kuhakikisha huduma ya TEHAMA inatumika kwenye maeneo hayo mfano kwa kutumia sehemu za mkononi  za kawaida.

 Wakala hiyo  ulianzishwa Julai mwaka 2012, ambapo taarifa mbalimbali za Serikali kutoka Wizara, Idara  , wakala na taasisi zake zitapatikana kupitia mtandao  wa wakala hiyo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...