https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Wednesday, October 09, 2013

Kituo cha afya Pongwe chalilia maabara, gari la kubebea wagonjwa wanaozidiwa na kutakiwa kuhamishwa haraka

Na Oscar Assenga, Pongwe   
KITUO cha Afya Kata ya Pongwe katika Halmashauri ya Jiji la Tanga kinakabiliwa na changamoto mbalimbali hali ambayo inapelekea kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea hasa katika utoaji huduma kwa wagonjwa wanaofika kituoni hapo.
Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Ally Bughe alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na mtandao huu ofisini  kwake na kueleza kuwa licha ya kuwepo hali hiyo lakini pia kituo hicho hakina uzio kitendo ambacho kinapelekea mifugo kuingia mpaka kituo wakati wa utoaji wa huduma.
Bughe alisema kituo hicho pia kinawakabili ni kukosekana kwa maabara ya kisasa kwa ajili ya kuchukulia vipimo vya wagonjwa licha ya kuwa na wataalamu wa kutosha.
Alisema licha ya kuwepo changamoto hizo wanatarajia kuanza kufanya upasuaji lakini hawana wodi maalumu ya kuwalaza wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji huo.
Aliongeza kwa kusema kuwa kituo hicho hakina gari maalumu la kubebea wagonjwa pindi wanapozidiwa na kuhitajika kupelekwa katika hospitali ya mkoa Bombo zaidi ya usafiri wa pick up ambayo sio salama kwao.
Aidha wanaiomba halmashauri ya Jiji la Tanga kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto hizo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi pamoja na kuhakikisha wanaondoa matatizo hayo.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...