https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, October 08, 2013

Matukio pichani katika mazishi ya baba yake msanii 20 percent

Abas Kinzasa kwa jina la usanii anaitwa 20 Percent akiwa kwenye majonzi baada ya kufiwa na Baba yake mzazi Mzee Kinzasa aliyefariki juzi siku ya Jumapili na kuzikwa siku ya Jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Hapa ndipo alikozikwa Mzee Kinzasa baba mzazi wa 20 Percent aliyefariki siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga.
Msanii 20 Percent na ndugu zake wakiweka udongo kwenye kaburi la marehemu baba yake mzazi mzee Kinzasa.
Abas Kinzasa kwa jina usanii anaitwa 20 percent akieleza jambo kandokando ya kaburi la  Baba yake mzazi Mzee Kinzasa aliyefariki siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga.

Marehemu mzee Kinzasa akiombewa dua baada ya kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele.
Hii ndio nyumba aliyoicha marehemu Mzee Kinzasa iliyoko kwenye kijiji cha Kimanzichana.
Baadhi ya wananchi waliofika msibani.
Wazee wakiesabu kiasi cha pesa kilichopatikana kwa watu waliotoa rambirambi zao kwenye msiba wa marehemu Mzee Kinzasa.
Mzee akieleza jambo kwenye msiba wa baba yake na 20 Percent aliyefariki siku ya Jumapili na kuzikwa nyumbani kwake kwenye kijiji cha Kimanzichana.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kimanzichana akimkabidhi mtunza pesa, pesa alizopewa na wananchi kwa ajili ya rambirambi.
Baadhi ya wananchi waliofika kwenye msiba wa baba yake na 20 Percent kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichoko wilaya ya Mkulanga mkoani Pwani hapo jana mchana.
Mtunza pesa akieleza kiasi cha pesa zilizopatikana baada ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika msibani hapo  kutoa rambirambi zao.

PICHA NA PAMOJA/PAMOJAPURE BLOG

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...