https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Saturday, October 05, 2013

22 wavishwa vyeo Jeshi la Magereza Tanzania, baada ya kupandishwa vyeo hivyo na Rais Kikwete

photoKamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(mbele kwenye Jukwaa) akipokea Salaam ya heshima toka kwa Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) katika hafla ya Uvalishaji vyeo kwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Magereza 22 ambao wamepandishwa cheo hicho tangu tarehe 19 Septemba, 2013 na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. Hafla hiyo imefanyikia leo Oktoba 05, 2013 katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga Jijini Dar es Salaam.imageKamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akimvisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Mnadhimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha kwa sasa, Injinia Jeremiah Nkondo. Sherehe hizo za uvalishaji vyeo zimefanyika leo katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Serikali(hawapo pichani).image (1)Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa wa Jeshi la Magereza katika hafla fupi ya Uvalishaji vyeo kwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Magereza 22 ambao wamepandishwa cheo hicho tangu  tarehe 13 Septemba, 2013. Hafla hiyo imefanyika leo katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya kupandishwa vyeo na Amri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...