https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Monday, October 21, 2013

Makamu wa Rais Dkt Bilal afungua Mkutano Mkuu wa 21 wa vyombo vya habari na utangazaji nchi za kusini mwa Afrika

Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal, alipokua akifungua mkutano huo leo Oktoba 21 2013 katika ukumbi wa A I C C jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) katika ukumbi wa A I C C jijini Arusha leo 21 Oktoba 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa  mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) baada ya kufungua mkutano huo leo 21 Oktoba 2013 katika ukumbi wa A I C C Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi mkuu wa TCRA Profesa John Mkoma nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C jijini Arusha, baada ya kufungua  mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) leo 21 Oktoba 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wasanii wa ngoma ya kimasai waliokua wakitumbiza  nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C jijini Arusha, baada ya kufungua  mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) leo 21 Oktoba 2013.Picha na OMR

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...